Maji Malamba Mawili Msikitini yaanza kutoka kila wiki

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Awali nilileta lalamiko la kutokuwepo huduma ya maji kwa muda mrefu bila sababu yoyote huku magari ya kuuza maji yakiwa yanaranda mitaani kuuzia watu maji kwa gharama kubwa.

Tazama hapa: KERO - Maji Malamba Mawili ni mgao mkali, baadhi ya Wakazi walio kwenye miinuko wana miezi hawapati maji kutokana na kasi ndogo ya maji. DAWASA wafafanua

Baada ya lalamiko hilo huduma hiyo imeanza kutolewa japo sio kila siku ila angalau mara moja kwa wiki maji yanatoka kwa masaa kadhaa angalau yamepunguza adha ya ununuaji wa maji kwa bei juu kwani watu hukinga na kuyahifadhi.

Your browser is not able to display this video.

Pamoja na kurejea, maji kutoka kwa wiki bado hayajfikia hitaji letu, tunahitaji jitihada zifanyike zaidi maji yawe yanatoka kila wakati bila kukatika kwani ni hitaji, na haki yetu kupata huduma hii muhimu na ya msingi kila wakati pasi na kupewa kwa siku na siku.

Sambamba na hilo asante sana JamiiForums Shukrani zangu za dhati kwenu kwa kupaza sauti zilozofika kwa walengwa ambapo awali walitolea ufafanuzi na kisha kuanza utekelezaji mara moja na kisha huduma kuletwa, mbarikiwe sana.

Pia soma ufafanuzi wa DAWASA baada ya lalamiko la awali: DAWASA yatoa ufafanuzi kuhusu changamoto ya maji Malamba Mawili
 
sawa ngoja kipindi cha uchaguzi kiishe utatupa tena mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…