Bendera kawaida ni utambulisho wa jumuia fulani au nchi na ni kitu cha heshima kabisa kwa jumuia au nchi inayohodhi bebdera hiyo. Kwa hiyo mtu anaposema amekunywa maji ya bendera ni kumaanisha kuwa yeye ni mtiifu sana kwa jumuia au chama kile kwa kiingereza watu kama hawa wanaitwa "die hard" wa jumuia na kama ni chi ndio hao wanaitwa "wazalendo halisi"
Hizi ni moja ya NAHAU
Yaani maneno au sentensi inayomaanisha tofauti kabisa na maana inayoonekana.
Kunywa maji ya bendera...hii inatokana na ukweli kwamba nchi au chama huwa na bendera maalum na hii ni utambulisho mkuu....hivyo kwa wale wazalendo (wafia chama/nchi) walipewa jina hili...yaani hata uwaue miili yao ina chembe (nutrients) za bendera...hivyo huwezi kuwatenganisha na chama au nchi husika.
Watu waliokiweka chama au nchi mioyoni mwao!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.