KERO Maji ya bomba yanazidi kuwa machafu kadri siku zinavyokwenda, DAWASA maji haya yana usalama kweli?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu kwema,

Maji yamekuwa yakitoka machafu kwa muda sasa, sasa hivi hali inazidi kuwa mbaya, maji ni machafu sana mpaka yanatia mashaka kwenye usalama wake, mbali na kuwa machafu kama hivi yana harufu mbaya pia kama vile kuna kitu kimeoza, japokuwa siyo strong sana lakini unaipata.

Kama maji tunayotumia ndio yana hali hii tutanusurika na magonjwa kweli? Nahofia inaweza kuwa tunakusanya magonjwa taratibu bila kujua maana unafungua bomba hata nusu saa maji yanayotoka ni machafu, mwishowe unaamua zako kutumia tu maana na bili inahesabika hapo

Ni sawa kulipishwa bili kwa maji haya kweli? Na maji unayofungulia ili yawe masafi si kwamba huyalipii, bili inasoma kama kawaida.

DAWASA mnatuhujumu wananchi, hii ni Mbezi Beach, maeneo mengine maji yenu yana hali gani, ukute ni pande hizi tu.

Wizara ya Maji

IMG_20240702_194451_340.jpg

====

Pia soma: Wakazi wa Mbezi Beach tunapata maji ya bomba machafu, na yana harufu mbaya. Mlipuko wa magonjwa unakuja
 
Nchi imemshinda kila kona malalamiko! Huo ndo kula kwa urefu wa kamba
 
Wakuu kwema,

Maji yamekuwa yakitoka machafu kwa muda sasa, sasa hivi hali inazidi kuwa mbaya, maji ni machafu sana mpaka yanatia mashaka kwenye usalama wake.

Kama maji tunayotumia ndio yana hali hii tutanusurika na magonjwa kweli? Nahofia inaweza kuwa tunakusanya magonjwa taratibu bila kujua maana unafungua bomba hata nusu saa maji yanayotoka ni machafu, mwishowe unaamua zako kutumia tu maana na bili inahesabika hapo

Ni sawa kulipishwa bili kwa maji haya kweli? Na maji unayofungulia ili yawe masafi si kwamba huyalipii, bili inasoma kama kawaida.

DAWASA mnatuhujumu wananchi, hii ni Mbezi Beach, maeneo mengine maji yenu yana hali gani, ukute ni pande hizi tu.

====

Pia soma: Wakazi wa Mbezi Beach tunapata maji ya bomba machafu, na yana harufu mbaya. Mlipuko wa magonjwa unakuja
Ni lini mwafrika ataweza kuwa mstaarabu na kufanya mambo ipasavyo? Tunakimbilia kukopa matrillion kujenga reli za kisasa SGR na mwendokasi wakati tunashindwa tu maji safi na salama. Hata kunya tu hatunyi ipasavyo. Pambaafff!
 
Wakuu kwema,

Maji yamekuwa yakitoka machafu kwa muda sasa, sasa hivi hali inazidi kuwa mbaya, maji ni machafu sana mpaka yanatia mashaka kwenye usalama wake.

Kama maji tunayotumia ndio yana hali hii tutanusurika na magonjwa kweli? Nahofia inaweza kuwa tunakusanya magonjwa taratibu bila kujua maana unafungua bomba hata nusu saa maji yanayotoka ni machafu, mwishowe unaamua zako kutumia tu maana na bili inahesabika hapo

Ni sawa kulipishwa bili kwa maji haya kweli? Na maji unayofungulia ili yawe masafi si kwamba huyalipii, bili inasoma kama kawaida.

DAWASA mnatuhujumu wananchi, hii ni Mbezi Beach, maeneo mengine maji yenu yana hali gani, ukute ni pande hizi tu.

====

Pia soma: Wakazi wa Mbezi Beach tunapata maji ya bomba machafu, na yana harufu mbaya. Mlipuko wa magonjwa unakuja
Hapo mbezi Beach je huko mbagala kwa kina adriz kukoje?
 
Karibia siku ya tano sasa maji yanatoka machafu sana, wahusika hawaoni hii hali au tunakomoana?

Chura kiziwi afungue hata sikio moja asikie tunachomwambia, maneno yake anayoongea bila kutafakari yanatuumiza watanganyika.
 
Back
Top Bottom