Naomba msaada wanaJF. Hivi mwanamke kumwekea maji mumewe bafuni ni wajibu au ni fadhìla tu? Nauliza hivi sababu mke wangu haniwekei maji mpaka nimgombeze au siku akipenda mwenyewe. Siku nyingi nalazimika kujibebea mwenyewe. Nimeshagombana naye mara kadhaa lakini habadiliki. Nifanyeje?
unajua museven, ngoja nikwambie kitu kimoja,
kwa mila na desturi zetu za kiafrika, hususan Tanzania..........
mapenzi na hayo maisha mnayoita romantic love ya mume na mke....
yameelekezwa zaidi katika majukumu, na wala sio katika muelekeo wa kizungu, ule wa kukisiana hadharani na kukumbatiana publically,
Having said that, mapenzi ya kiafrika yameboreshwa zaidi na majukumu yanayofanywa na wanandoa wenyewe...
na ni kwa jinsi gani , jamii inavyochukulia na mafundisho au aina ya maisha ambayo wanandoa wenyewe wamekuzwa nayo....
kitanzania, mwanaume anaonekana kichwa cha nyumba
na ataonekana ni mwanaume halisi anaeipenda familia yake na kumjali mkewe,
kama tu anatekeleza wajibu wake wa kimsingi, yaani kumjali mke wake kwa lishe, afya, mavazi na mahitaji mengine ya kimaisha,
kumbuka kuwa hapa, unaweza usionekane ni baba bora kama tu unadhani kwa kumkiss mkeo kila wakati, kumhug na kumshika mikono kwa mbwembwe, ndio suluhisho...........wakati mambo ya kimsingi katika maisha hujayatekeleza.
kwa wanawake, kule kumjali mumeo, kwa mambo kama hayo aliyosema museven, yaani kuweka nyumba katika usafi, kumwandalia mumeo maji ya kuoga, kuongea nae kwa lugha ya mahaba, kumheshimu,kumwandalia chakula kizuri ndo ya msingi sana.
Kitanzania bado hatuoni kuwa mwanamke anaejua kukata kiuno na kukupelekesha kwenye kungonoka ndo mke bora........hpana hii dhana kwenye jamii yetu bado ni ndoto!.......na hii ni sababu ya mfumo wa kimaisha tunaouishi...............
Lo.......nilisahau kuwasalimia wapendwa wangu!habari za masiku tele wapendwa, JF, long time............................
nipo nimefichwa huku South Sudan, karibuni kwa tahadhari lakini.
Tchaooooooooooooooooooo.................