Nitangulize shukrani kwa JamiiForums kwani mara tu bada ya taarifa ya kukosekana kwa maji kuripotiwa mamlaka zimeweza kurejesha huduma ya maji katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani kijulikanacho kama Magufuli stendi.
Awali nilileta uzi wa lalamiko la kutokuwepo kwa huduma ya maji kwa muda wa siku mbili, unaweza kusoma hapa: Stendi ya Mbezi Magufuli hakuna maji siku ya pili leo
Maji yameanza kutoka na hali ya stendi itarejea katika hali ya kawaida na kuondokana na adha iliyokuwa imeikumba kwa muda wa siku mbili wa kukosekana kwa maji hali iliyokuwa imesababisha huduma ya vyoo kuzuiliwa kwa watu wanaotaka kufanya "long call" na hata wa haja ndogo kulazimika kununua maji ya chupa au tishu ili waweze kujihakikishia usafi wao hasa kwa wa kina mama.