Peter Msigwa ni mwanasiasa ambaye aliwahi kuchaguliwa kuwa mbungi wa jimbo la Iringa mjini kuanzia mwaka 2010 hadi 2020 kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Juni 30, 2024 Msigwa
alijiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM NEC kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan. Msigwa pia ni miongoni mwa
watia nia wa ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM.
Balozi
Humphrey Polepole ni wanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye amaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba.
Julai 18, 2025 Balozi polepole alifanya mkutano na waandishi wa habari mbashara kupitia ukurasa wake wa
Facebook ambapo pamoja na mambo mengine alikosoa vikali utaratibu uliotumika kumpata mgombea wa Urais pamoja na makamu wake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
akisema 'Wakati mwingine inabidi tubomoe ili tujenge. Mchakato wa kupata wagombea tumeukosea'
Picha ya majibizano ikiwahusisha Balozi Polepole na Mchungaji Msigwa.
Ipo picha ya majibizano inayosambazwa katika mtandao wa Facebook ikionesha Peter Msigwa na Balozi Humphrey Polepole wakijibizana katika sehemu ya maoni kupitia mtandao wa X ambapo Polepole anamtaja Msigwa kutumiwa kama pandikizi kipindi alipokuwa CHADEMA.
Je, ni upi uhalisia wa picha hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa ujumbe huo si wa kweli ni wa kutengenezwa na wapotoshaji kwani haujachapishwa
Peter Msigwa pamoja na Balozi Polepole kwenye mtandao wa X.
Yapo mapungufu kadhaa yanayodhihirisha kuwa jumbe hizo ni za kutengeneza kwani picha hiyo haiakisi uhalisia kama ilivyo katika mtandao wa X. Mathalani kutokuwepo kwa alama inayoonesha idadi ya watu waliofikiwa na maoni hayo, kukosekana kwa alama ya Grok, pamoja na alama ya kuhifadhi ujumbe 'Bookmark'