gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,312
- 3,345
Magufuli anaposema watu wameficha pesa ndani hakurupuki.
Jana tumesikia raisi akitishia ku print pesa mpya ili kuwatia hasara wale wanaomuhujumu kwani mazingira yanaonesha kuna watu wameficha pesa majumbani kwa makusudi ili kuleta hitilafu zakiuchumi hewa,hizi ni hitilafu hewa kwani BIOT wanapofuatilia pesa zilizo ruhusiwa kwenye mzunguko wataona zipo kwenye kiwango kinachohitajika lakini mtaani wananchi wanapiga kelele pesa hakuna.
Tukubali tukatae matajiri wakubwa kadhaa wakiamua kuzibana pesa zao majumbani ni lazima uchumi utatikisika na hata kutokea deflation kali na yenye madhara kwa mwananchi mmojammoja.
Juzi hapa tumeshudia Tanzania ikikumbwa na uhaba wa sukari lakini ilikua inasekana(uvumi) aliyesababisha tatizo lile ni super dealer bw Za.karia.Wengi watasema sera za Magufuli lakini huyu jamaa alikua na mchango mkubwa sana kwenye sakata lile.Ni tajiri mmoja tu lakini aliitikisa nchi.
Kuna watu wanasema pesa hakuna mtaani kwasababu mafisadi waliamua kununua asset kama viwanja na majumba yakifahari ndio maana pesa hakuna.Hoja hii haina mashiko kwani kama hizi asset zimenunuliwa ndani ya nchi hii ni currency circulation ya kawaida ya ndani tafsiri yake ni kwamba pesa imehama kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ndani ya nchi hivyo ilipaswa kuwepo.
Kuna watu wanasema pesa hakuana mtaani kwasababu mafisadi walipoona raisi hatabiriki walihamishia pesa nje ya nchi.Hili nalo haliwezekani kwani nje ya nchi watu hawahamishi madafu(tsh),kama kweli chanzo ni hiki basi nchi ingepata changamoto ya akiba ya dola kwani ndio zingepungua nchini.Tafsiri yake ni kwamba kama mtu alikua na tsh akitaka kuhamisha lazima a change kwanza kutoka tsh kwenda dola hivyo iko palepale kwamba angeacha tsh nchini na kuondoka na dola.
Kuna watu wanasema pesa hakuna kwasababu serikali inazo yenyewe kwani sasa wanakusanya kodi sana na huku imebana matumizi.Hapa kama chanzo ni hiki Raisi asingepiga kelele.Lazima ifahamike raisi kupitia BOT hasa kutokana na sasa account zote za serikal pamoja na taasisi zake zipo BOT,BOT inafahamu kiasi cha pesa ambazo serikali imezikumbatia kwa sasa,lakini pia BOT inafahamu imerusu kiasi gani kwa ujumla kuingia kwenye mzunguko na inapotizamwa inaonekana kabisa kwamba ukiondoa pesa ambazo serikali imezikumbatia kwenye account zake bado kunatakiwa kuwe na pesa mtaani,lakini sasa hakuna,pesa iko wapi?
Kama pesa hizi zingehifadhiwa kwenye ma bank,mabank yasingelalamika ukata uliopo sasa.
Watu wanalalamika pesa hakuna,Ma bank yanalalamika pesa hakuna,hii pesa imekwenda wapi kama si ipo majumbani kwa matajiri wa chache?
Hitimisho.
Ni dhahiri nje ya hujuma,sio rahisi mtu akihifadhi tsh ndani kwani tsh haiko stable hivyo kwa vyovyote vile kama mfanya biashara akiamua kuhifadhi pesa zake kwakuhofia usalama wa pesa zake kutokana na sera za serikali ya awamu ya tano lazima ahifadhi dola na si tsh kwani dola mara nyingi iko stable na hupanda thamani hivyo ni faida mtu kuhifadhi dola badala ya tsh ambayo wakati wowote inaweza kushuka thamani.
Yeyote aliehifadhi tsh ndani mpaka kupelekea hii nakisi inayoonekana sasa huyo analengo la hujuma na hila kwa serikali ya awamu ya tano kwani anachokifanya hakina faida kwake na hapa ndipo raisi yuko sahihi anaposema kwamba kwa vyovyote atakua anahujumiwa.
Kuhifadhi pesa nyingi ndani ni risk mfano wizi na majanga ya moto,lakini mtu amediriki kuzihifadhi ndani kwa faida ya nani kama sio kumkomoa Magufuli?