RAiSI KUBADILI NOTI SIO SUlUHU
Mnamo hapo jana MH.JP Magufuli alitishia
kubadili noti ili kuwakomesha wale waliozificha
lengo ni kuwataka waweke fedha benki ili ziingie
kwenye mzunguko. Kisiasa ni rahisi sana kufanya
hivyo ila ni kiuchumi ni vigumu sana kufanya
hivyo.
Kumbukumbu zinaonyesha ili fedha ipotee
kwenye mzunguko inachukua zaidi ya miaka
mitano na kuendelea which means hata Noti
zikibadilishwa leo bado wale waliozificha
wataendelea kuzitumia mpaka Mwaka 2021 kwa
mantiki hiyo tatizo la upotevu wa fedha kwenye
Taasisi mbalimbali za kifedha halitatatuliwa
kirahisi.
Fedha kwenye mashirika ya fedha ipotelea wapi?
Mojawapo ya maswali magumu ambayo
watanzania wengi wameshindwa kuyaelewa kwa
kina ni wapi fedha imepotelea.
1.Ongezeko la kodi kwenye miamala ya fedha
(increase in transaction cost). Serikali
ilipotangaza ongezeko la kodi ya ongezeko la
thamani (VAT) iliwaathiri moja kwa moja
watumiaji wa sarafu ya shilingi. Mfano rahisi
Asilimia 18 ilioongezwa kwenye bei ya kufanyia
miamala ilipunguza kwa kiasi kikubwa Bank
deposits za watu kitu kilichopelekea pesa nyingi
kurudi mikononi mwa watu na benki nyingi
kukosa pesa kwa ajili ya kufanya shughuli za
kifedha nchini. Hapo utaona aienufaika ni TRA
kwani mapato yameongezeka kwa asilimia 18 ya
kila muamala anaofanya mtu mmoja.
2.Ongezeko la bei za vitu muhimu kama sukari.
Ugumu mwingine uliosababisha fedha ipungue
benki na kurudi mikononi mwa watu imechangiwa
kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kiholela kwa
bei ya sukari which means sukari iliokua inauzwa
sh.2000 ilipanda hadi Zaidi ya shilingi
2700,matokeo yake kiuchumi Ilipunguza kwa kiasi
kikubwa pesa mikononi mwa watu kwa zaidi ya
asilimia 40 na kupelekea pesa benki kupungua
kwa asilimia zaidi ya 40 kwa kila kilo ya sukari
ilionunuliwa.
3. Serikali kubana matumizi(Reduction in
government expenditure). Hapa napo tulifeli kwa
kiwango kikubwa serikali ilibana matumizi
yaliosadikiwa sio ya lazimaa,hapa napo pesa
badala ya kwenda kwenye mikono ya watu wengi
iliishia kwenye mkono mmoja wa serikali hivyo
kupunguza kiwango kikubwa cha pesa kwenye
mzunguko
4.Kodi kubwa na mizigo kwenye sekta ya utalii
na bandarini. Mwezi uliopita iliripotiwa kua
Magari kwenye bandari ya Dar es salaam
yamepungua kutoka magari 3000 hadi magari
1500 kwa siku moja,na hii ilisababishwa kwa
kiasi kubwa na ongezeko la kodi huku serikali
ikidhamiria kukusanya mapato mengi ndani ya
muda mfupi.Hapo tulifeli kwa kiasi kikubwa kwani
tunazungukwa na nchi washindani wenye bandari
kubwa kuliko yetu kwa Mfano Msumbiji na
kenya.Wafanya biashara wengi wamekimbilia
huko kwa hofu ya kupata hasara,madhara yake ni
watu wengi kukosa ajira na hivyo kupelekea
kukosekana kwa ujira ambao ungeweza kuongeza
pesa kwenye mzunguko.
Nini kifanyike sasa?
Ni dhambi kubwa kuwakomoa watu waliojiwekea
fedha walizotafuta kwa jasho lao wenyewe na
hata sarafu ikibadilika bado hawataweza
kuathirika moja kwa moja. Serikali ingejitahidi
kuongeza idadi ya pesa nyingi kwenye mzunguko
kwa kutumia benki kuu ya Tanzania. Hapa Benki
kuu inatakiwa kununua bonds kutoka kwa watu
binafsi na mashirika ya watu binafsi ili ku
dispense more amount kwenye mzunguko, pili
kodi zisizo za msingi zipunguzwe ili
kuwashawishi watu waendelee kutumia mashirika
ya kifedha. Benki ni kama mfanyabiashara tu
ambae yupo pale kwa ajiri ya kujipatia faida sasa
ukiongeza kodi ina maanisha mtu wa mwisho au
benki yenyew inaweza kubeba mzigo mzito
ambao ni vigumu kuutua na utaangukia uchumi
wa nchi nzima (Macroeconomics)
Owen j chimela