Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

Aliiba kura mwaka jana bana, hata kama tungepiga kura watu laki 4, kura zikahesabiwa kwa haki na akatangazwa aliyepata kura nyingi ndo mshindi KIKWETE ASINGESHINDA, ila jamaa(JK) anatu-cost jameni, lets do something, pls
 
We still have a chance, but I see people don't want to use this chance we have now!! Tunasubiri hadi kila kitu kigome ndo tuamke.
 
Nafkiri mtu kama kikwete kuwepo madarakani hadi sasa says something about US! ME AND YOU!
Na the best thing to do ni kuto subiri uchaguz bali kujaribu kumngoa sasa,hata tukishindwa mpaka hio 2015 itakua fundisho kwa anaeingia kuwa mitanzania ya sasa sio ya mwaka 47!
 
wewe mkuu mpaka umuone kwa TV? mie nikiona tu jina Kikwete du naanza kucheka sana, sometimes hata nikiona tu herufi mbili za mwanzo Ki...tayari kicheko hicho
ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha...
 
Tatizo letu watanzania ni namna tunavyowapata viongozi. Kupata uongozi hapa nchini ni sawa na kucheza "TOMBOLA" kila mtu anaweza kuwa kiongozi...hii ndio tofauti yetu ya msingi na walioendelea.
 


Haapa nasoma lawama tupu. Ningekuona tofauti na Kikwete kama angalau paragraf moja ungetoa mapendekezo ya ufumbuzi wa tatizo la umeme TZ, AMA LIWE LA MUDA MFUPI AU LA KUDUMU.

Huwa napata kichefuchefu kusoma taarifa kama hizo kwani hazina tija wala faraja. Isitoshe zinaonyesha jinsi watanzania au kwa ukika zaidi wanaJF wanavyofanana akili zao. Baya zaidi ni kila utapofungua mada utakuta hali hiyo hiyo hata kwa wale tuliowaamini sana na kuwaita WASOMI WA JF.

Kweli NYANI HAONI KUNDULE!
 
Ha ha ha mzalendo umenifurahisha sana kumbe tupo wengi!!!!!!!!!!!!!
 
Huyu jamaa alikuwa Mbunge wa Chalize kwa miaka kibao kaiacha haina sekondari hata moja ukiondoa ile ya Lugoba aliyosoma yeye middle school atawezaje kuwa na maono ya maendeleo kwa taifa?
 
Katika majibu yake Kikwete alionyesha 600MW tangu uhuru na hizi 300MW wanazoziongeza, labda tu niwajuvye wakati ule 600MW zilikuwa over and above mahitaji ya umeme na hivyo kuwa excess reserve, mgao wa umeme Tanzania umeanza miaka ya late 90's precisely 97

Hivyo kwanza ni kushukuru awamu 2 za mwanzo kwa kuwa na reserve, nchi nzima ni kama 300MW tu zilizohitajika na si zaidi!!

Awamu 2 zilizofuatia kasi ya ukuaji wa uchumi, uwekezaji na access to electricity imeshika chati, hivyo haiingii akilini kurudi kwenye zama za mawe za awamu 2 za kwanza kwani hazifanani kabisa, maeneo mengi yamebadilika kila kukicha majumba yanajengwa mijini na vijijini , viwanda vipya vinaingia, migodi na kadhalika, katika mipango hii yote huwezi kuacha kukipa kipaumbele umeme kiutaalamu na si kwa kusoma 600MW za miaka ya 80's

Mgodi mkubwa kama Geita hautumii umeme wa TAnESCo pale mahitaji yao ni 40MW,maghorofa yote mazito mazito yanayoporomoshwa mijini hayo mahitaji ni @least 2MW , hujahesabia viwanda nk nadhani ukifanya demand side management utaona mahitaji yanakua kwa 100MW kwa mwaka tangu 2005 hiyo inatosha kuonyesha serikali haiko makini kuwaza 600MW za nyuma na kujisifia kwa 300MW za sasa
 
Tatizo la huyu mtu ni ujuaji, anajua kila kitu, na hili ndilo linalopelekea haya yote, inaoneka hashauriki.
Wakati anapojibu maswali sijui anafikiria wapi, yaani yupo yupo tu, cha kushangaza akishastaafu utasikia eti nae anabusara.
Kuna matukio mengi yanayoonesha dharau zake, kama ulipata kuona mahojiano wakati wa kampeni bukoba ailijibu kwa dharau sana.
Nasijui anatoa wapi jeuri hii, lakini ukweli unabaki wazi kuwa huyu mtu ana IQ ndogo.
 
Huyu jamaa alikuwa Mbunge wa Chalize kwa miaka kibao kaiacha haina sekondari hata moja ukiondoa ile ya Lugoba aliyosoma yeye middle school atawezaje kuwa na maono ya maendeleo kwa taifa?

Hata za kata hakuna?????????
 
Jeyi Keyi anaitaji maombi ya nguvu!!!!!!! "I need Meditation so i can lead my people"-The game
 
Kwakweli kikwete kama ni zarau zimepitiliza rais hatakiwi kuwa hivyo, wananchi tunalia tatizo la umeme yeye anaongea kabisa pumba zake kwa kujiamini huku anacheka, inasikitisha sana na inauma sana kwa alichokijibu kikwete bora mnao hadisiwa kuliko 2lio mshuhudia kwa kuacha kazi ze2 eti 2namsikiliza rais
 

Baelezee Engineer.

Lakini...hivi hatuna qualified Engineers pale TANESCO??
 
Wana JF.

Nadhani JK amerudisha ile kauli ya RUKSA kila mtu achukuwe na afanye atakavyo sasa
 
Nikimwangaliaga huyu Mkwer.e kwenye TV naishia kucheka tu! Nadhani mnajua sababu.
mchungaji wewe unauvumilivu mimi huwanatamani kuvunja tv kabisaa kwa hasila nachofanya nikubadili channel tuu!
 
Sipendi kuitwa mkabira lakini na hii inabidi kuwa kati ya vitu vya kuviangalia kuteuwapo wagombea nafasi za Urais. Sasa kama Rais atatokea kwenye kabila ambalo mila na desturi zao hazioni hasara ya kuuza ardhi au makazi yake Mazuri, yalio sehemu mzuri iliyo mjini kwa mgeni na yeye akawa tayari kuhama kwenda sehemu ya mashambani isiyo na maendeleo. Unategemea nini si kama atauza Raslimali za Nchi kwa wageni na kutona tatazi lolote kama wananchi wake watakosa umeme kwa ajili ya kujiendeshea maisha yao na uchumi wa nchi yao.

Kama nilivyosema sipendi kuwa mkabila lakini mila na desturi zituelekeze kwani kuna mila ambazo huwa zinalinda sana raslimali yaani KIAMBA, hebu jaribu kumdhulumu mchagga, mhaya, myakyusa kipande kidogo tuu cha ardhi au mkurya, mmasai, mnyamwezi mdhulumu ng'ombe utaona moto wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…