Majibu ya kisheria: Je, ni kweli mwanaume akiishi na mwanamke kwa kipindi kirefu wanakuwa wameoana?

Utaratibu nikuwa mgawanyo unategemea na uchangiaji wa kila mtu kwenye familia mahakama wanatoa kwa asilimia kwa hiyo wanaweza toa 20 kwa 80 au 40 kwa 60
 
Mali mtakazo gawani Ni zile tu mlizo chuma pamoja yaani mfano umeishi nae toka 2012 tunaweza sema mali ulizoanza pata mwaka huu mpk leo mlizichuma pamoja
 
mkuu naomba kuuliza kwa.muislam subsisting marriage akiwa anaishi na.mwanamke mwengine inamhusu mwanaume wa kislam na hususan wameruhusiwa wake wanne
 
Mali mtakazo gawani Ni zile tu mlizo chuma pamoja yaani mfano umeishi nae toka 2012 tunaweza sema mali ulizoanza pata mwaka huu mpk leo mlizichuma pamoja
Niulize jambo kupitia hili jibu lako tafadhali...

Mwaka 2010 nimempa mimba mdada, akaendelea kuishi kwao, ilipofika mwaka 2014 ndugu wakalazimisha kwenda kujitambulisha ukweni (mimi sikwenda)

Baada ya hapo, mwaka 2015 mama mtoto akaja kunitembelea (tunaishi mikoa tofauti), alipokuja tukafanya mapenzi, akachukua mimba na kuondoka!

Mtoto akazaliwa 2016, akamleta mtoto mwaka 2017, akakaa mwezi mmoja na kuondoka!

Baada ya hapo hakuwahi kuja tena, (lakini mwaka 2016 akiwa mbali nilinunua kiwanja, n'a yeye kwa hiari yake alinichangia sh.milioni 1 kati ya mil 4.5)

Tangu hiyo 2017 hakuwahi tena kuja kwangu, ni baada ya kupata jamaa mwingine na kuzama penzini!

Na toka hiyo 2017 nilinunua viwanja, mashamba n.k, na kiwanja alichochangia mil.1 pia nilikijenga na kuanzisha mradi ambao mpaka sasa unaniingizia pesa!

Sasa mwaka jana 2023, niliamua kuoa, mtu ambaye naye ana mtoto wangu tayari, yule wa mwanzo aliposikia ninaoa amekuja juu kwa fujo, anadai kugawana mali zote hana mchango nazo kwa namna yoyote zaidi ya milioni moja yake aliyonichangia wakati nanunua kiwanja.

Swali ni je, mbele ya sheria, anayo haki ya presumption of marriage?

Na je, mbele ya sheria kama anayo haki kutokana na mchango wake wa mil.moja inafanya awe na haki kwa vitu vingine vyote nilivyofanya bila uwepo wake wala mchango wake?
N.b tuna watoto 2, ila hatujawahi kuishi pamoja kwa hata miezi 3 mfululizo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…