Vuta subira dogo. Labda wazazi hawakufahamu vizuri tabia yako ndio kwanza ametumwa shushushu ili aone kama kweli ww unafaa kuoa. Au kimeandaliwa kikao cha wazee wa familia ili wapange kiwango cha mahari kulingana na mila zao. Ila kama tayari umeshapachika mimba hakuna kikao, utapewa jibu la kupeleka ng'ombe wa faini. Ili usiwe na mawazo sana fanya utafiti wa kiinterijensia kutoka kwa huyo mkeo mtarajiwa, maana ni lazima yeye ataanza kuulizwa kama anakupenda kwa dhati, na jibu la awali utalipata kutoka kwake.