Majibu yangu kwa Baba Askofu Stephen Munga kuhusu Bandiko lenye kichwa cha habari kisemacho "CHADEMA JITAFAKARINI"

Ukweli mchungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Yaani hiki chama ni Cha ovyo kwelikweli
 
kipande,
Ndugu, kuhusu kugombea kwa Mbowe ni takwa la kikatiba, unataka tuvunje katiba kwakumzuia mwanachana asigombee?
Hivyo "CCM" kwa mfano, wakifanya marekebisho ya katiba na kuondoa ukomo wa urais itakuwa sawa kwa say, Magufuli kutawala milele kwa kuwa ni matakwa ya kikatiba! Hiyo ndiyo demokrasia mnayojinasibu kuiamini?

Hivi juzi baada ya Mashinji kuondoka kiongozi wa BAWACHA Mdee, amenukuliwa akisema "sasa mmeelewa ni kwa nini tuliwafyeka baadhi ya watu". Sasa kwa mwendo huo mnamdanganya nani kuwa mnajenga chama na si kitaasisi cha kuchukulia ruzuku?

Kwa siye wengine tuliokuwa wafuasi wenu wa kutupwa tunaumia sana mnavyozidi kukipeleka hicho chama akhera.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema wanang'ang'ania tu ligi ya ndondo hawawezi kucheza ligi kuu.

Hiki Chama huwezi fahamu falsafa yake hata siku moja, wanajificha tu nyuma ya madhaifu ya CCM
 
Ndugu Chadema inaongozwa na Katiba ya Chadema sio Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katiba yetu inampa uhuru mwanachama yoyote kugombea hakuna ukomo, na uchaguzi ni kila baada ya miaka mitano.
 
Hivi unafahamu tofauti ya Katiba ya Chama na Katiba ya Nchi?
 
Mkuu Yericko, unataka tuanze kutaja majina humu, au kwa vile unajua kuwa mimi nilimzimikia yule dada cheupe na nikampigania sana hadi humu, hivyo unauliza majina ili nimtaje watu wanijue nilivyo mdhaifu kwa watu fulani fulani?, no simtaji yule, tuanze na Zitto akiwa NKM wa Chadema
1. Mamlaka ya nidhamu ya NKM ni ipi?
2. CC ya Chadema ilipomfukuza, ulitumia mamlaka gani kwa mujibu wa katiba ya Chadema?.
3. Mtu kujiunga na chama anajiunga kwa barua na kufukuzwa kwa barua, find out from Chadema, kama kuna any letter on record ya kumvua Ziito uanachama?.

P
[/QUOTE]
Hahahaa kwanza nisamehe kwa kukukumbusha juy ya dada mweupe uliyempenda na unayempenda,

Umeamua kuchukua kesi ya Zitto kama mfano hai wa kujenga hoja yako.

Kwakukusaidia na kuwasaidia wasomaji na wanachama kwa ujumla, Kamati Kuu ya Chadema haijawahi kumfukuza Zitto uanachama, bali ilipendekeza/ilielekeza adhabu kadhaa ambazo zilitakiwa kwenda kupata baraka na Baraza Kuu, na wakati utaratibu wa Baraza kuu ukiendelea, Zitto alikwenda Mahakamani kukishitaki Chama, na kwamjibu wa Katiba ya Chadema, mwanachama atakayepeleka mashauri ya kichama mahakamani huyo atakuwa amekosa sifa za kuendelea kuwa Mwanachama hai. Hivyo uanachama wa Zitto ulikoma automatic alipofungua kesi mahakama kuu.

Hapo kifungu gani cha katiba kilikiukwa juu ya kesi hii?
 
Chadema wanang'ang'ania tu ligi ya ndondo hawawezi kucheza ligi kuu.

Hiki Chama huwezi fahamu falsafa yake hata siku moja, wanajificha tu nyuma ya madhaifu ya CCM
Mwanaccm uliyeko katika box pale Kumumba utajuaje falsafa ya Chadema ndugu ikiwa hujishughulishi kujua?

Kwakukusaidia falsafa ya Chadema ni Nguvu ya Ummaa au Peoples Power
 
Nyie mkikosolewa mnakuwa mbogo kweli, alafu baadae mnasema JPM hataki kukosolewa! Hivi nyie mngekuwa na dola wakosoaji wenu mngewafanya nini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Acha kutaka kupotosha maana, hapo huyo askofu amekosoa na amejibiwa, umeona katekwa, au kubambikiziwa kesi? Au ulitaka huo ukosoaji wa askofu umezwe kama ulivyo?
 

Tume huru ya Zanzibar ilikuwa inaenda kumtangaza mshindi halali, kama Kawaida dola ikachafua uchaguzi, tushukuru Mungu damu haikumwagika. Kenya pia tuliona mpaka kesi ikafunguliwa mahakani kupinga matokeo ya uchaguzi. Na ukitaka kujua tume huru maana yake nini, je umeona katika hizo sehemu zenye tume huru chama chochote kikipata ushindi wa kishindo? Ni hivi wewe una nongwa na cdm ndio maana unarukia hoja mfu kama za chama kutaka ruzuku ili kung'arisha hoja zako. Suala la tume huru wala halina mjadala, na usitake kuleta upotoshaji ukitegemea huo utetezi wako dhaifu utapindisha ukweli.
 

Huwa akiikosoa huko upande wa pili huwa mnamsifia? au hizo kejeli mnazoandika mnadhani huwa hatuwezi kuzisoma? Kumbuka hili ni jukwaa huru na sio ofisi ya chama chochote cha siasa, hivyo kila mtu ana maoni yake. Kwa hiyo usije na maoni yako kama kwamba hapa kuna maoni ya chama fulani rasmi.
 
Hujawahi kuijua Chadema. You can't tell the folk tale
 
Yericko hukupaswa kuwa mwanachama wa Chadema hii ya matusi, you are too intelligent to be one of them,

sijui kama nimeandika kiingereza fasaha.
 
Kwani CHADEMA wanaongozwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano kwenye mambo yao ya kichama ?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
sikujua Yericko Nyerere ni mjengaji mzuri wa hoja kiasi hiki.

umemjibu vyema sana huyu mwana CCM wa madhabahuni!!
 
Yericko Nyerere na kinyonga ni baba moja mama moja. Leo hii itokee Mbowe aache Chadema Yericko ataandika uzi mrefu saana. Huyu mla mbwa nadhani alikula kajibwa kagonjwa. Ukiangalia nyuzi zake kuhusu Lowasa zimegawanyika sehemu tatu. Halafu hanaga hata aibu huyu mtu.
 
Shida yenu hamtaki ushauri au kukosolewa na mnataka msifiwe tu,matokeo yake ni kuwa mtabaki na akina Lema ,Bulaya(CCM) na shoga wake Halima,Sugu,Msigwa, na wapambe wengine wa Dj Mbowe
Hiyo sawa lkn na nyie acheni basi mambo ya utekaji, utesaji, uuwaji na wizi wa kura ili basi kama ni kushinda mshinde kihalali ili hivi vijembe vya humu viishe. We're tired of perennial stratagems.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…