SoC01 Majigambo ya nahodha na dereva

SoC01 Majigambo ya nahodha na dereva

Stories of Change - 2021 Competition

GoJeVa

Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
41
Reaction score
60
MAJIGAMBO YA NAHODHA NA DEREVA.


NAHODHA:
Kazi ya majasiri..!!!

Unahodha kazi nzuri, mtumbwi naendesha,

Kwa nyuma naukalia, mawimbi naachanisha,

Raha kisogoni naisikia, kasia langu kupigisha,

Unahodha kazi nzuri, wengineo jifunzeni.

DEREVA:
kazi yenye heshima…!!!

Udereva ni heshima, wengi tunajua,

Usukani nakamata, kwa mbele nashikilia,

Macho nakodoa, gia nakanyagia,

Udereva kazi nzuri, watu wote karibuni.

NAHODHA: mtumbwi hutuli..!!!

Kwa nyuma nikishikilia, chombo hutulia,

Kwa mbele nikikalia, mtumbwi hupotea,

Mtumbwi hauendi mrama, hakika najisifia,

Unahodha kazi nzuri, wengineo jifunzeni.

DEREVA:
gia naingizia..!!!

Njia safi napita, krachi nashikilia,

Kwa nyuma si maadili, siti mbele nakalia,

Nashangaa nahodha, nyuma kung’ang’ania,

Udereva kazi nzuri, watu wote karibuni.

NAHODHA: dereva hukosea..!!!

Dereva hukosea, kwa mbele kukalia,

Nashindwa muelewa, balansi kupatia,

Dereva karibu, kwa nyuma anza kalia,

Unahodha kazi nzuri, wengineo jifunzeni.

DEREVA:
nahodha hapana…!!!

Kwa mbele zingatia, haya yetu maadili,

Kwa nyuma epukeni, tutumie zetu akili,

Wageni kutuletea, kuaribu zetu adili,

Udereva kazi nzuri, watu wote karibuni.

*UFAFANUZI WA MWANDISHI KWA UFUPI.

Hapo juu ni mfano wa majigambo, majigambo haya yanahusisha wahusika wawili ambao ni dereva na nahodha. Dereva anasifia vile anavyoendesha gari wakati nahodha pia anasifia huendeshaji wake wa mtumbwi. Kama tujuavyo katika kuendesha mtumbwi nahodha hukaa nyuma ya mtumbwi na katika kuendesha gari dereva hukaa mbele, hapo lugha ya kifasihi imetumika ili kumfikirisha msomaji. Dhamira kubwa ya majigambo haya ni kupinga suala la mapenzi yafanyikayo kinyume na maumbile, tunaona nahodha anahamasiha suala la kuingiliana kinyume na maumbile lakini dereva amekemea suala hilo na kusema sio tabia nzuri wala sio maadili yetu. Wewe kama hadhira, soma kwa makini majigambo hayo ili ufikirishe akili na ujifunze zaidi. Fasihi ni zao la jamii. AHSANTENI.


Tupinge mapenzi kinyume na maumbile.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom