Majimaji yaapa kufa na Yanga

Majimaji yaapa kufa na Yanga

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Majimaji.jpg

Klabu ya soka ya Majimaji ya mkoani Ruvuma imejinasibu kuwafunga mabingwa watetezi wa VPL Yanga kwenye mchezo wao wa kesho.

Majimaji kupitia kwa mjumbe wake wa kamati ya utendaji Salum Masamaki wamesema wamejiandaa vyema chini ya mwalimu Habib Kondo na wanaamini watapata ushindi katika mchezo wao wa kwanza kwenye uwanja wao wa nyumbani.

"Tumejiandaa vyema na mchezo tutaifunga Yanga bila shida kwasababu timu yetu iko vizuri ndiyo mana tumetoa sare moja na kupoteza mchezo mmoja lakini michezo yote tumecheza ugenini", amesema Masamaki.

Katika hatua nyingine Masamaki amethibitisha kuwa kocha wao Kally Ongala hayupo na timu kwasababu mkataba wake unamalizika mwezi Oktoba hivyo bado anaongea na wadhamini ambao ni GSM ili kuona kama ataongeza mkataba.

Majimaji ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa VPL ikiwa na alama moja baada ya michezo miwili na itakuwa nyumbani kesho kucheza na Yanga kwenye raundi ya tatu.

EATV
 
kesho utasikia tu vituko vya yanga mara waingilie mlango tofauti, mara wagome kuingia dressing room yaani full vibweka maana shughuli wanaijua kila wakija songea kucheza na majimaji. kila la heri majimaji tusiposhinda basi hata sare.
 
Yanga hata wakamilike vipi ila wanapokuja kucheza kucheza uwanja wa majimaji wanaambulia sare au kufungwa,na endapo ikishinda goli lazima liwe la utata
Ni hayo tu mwanayanga kindakindaki kwa sasa nipo pyopyung
 
Back
Top Bottom