Kinjekitile junior
JF-Expert Member
- Apr 20, 2015
- 4,404
- 581
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha jana kupitia ITV kwenye taarifa ya HABARI YA SAA 2 Usiku mmoja wa viongozi wa UKAWA aliweka wazi kuwa ndani ya UKAWA kuna mgongano wa kimasilahi kwenyenmajimbo ya uchaguzi 12 hali iliyowafanya kushindwa kuafikiana juu ya hatima yao kuelekea kwenye uchaguzi mkuu!
UKAWA wamekuwa mstari wa mbele sana kushambulia madhaifu ya upande mwingine hasa wa Serikali na kusahau kabisa ndoa yao waliyoifunga mwaka jana ambayo iko rehani kwa sasa kwa sababu tu ya kushindwa kuafikiana kwenye majimbo 12 sijui nini kinawafanya wasikubaliane!
Kwa kuendelea kuendekeza ubinafsi na tamaa ya madaraka waliyo nayo naanza kupata wasiwasi kama wanatutetea vyema kwenye masuala serious ya nchi, kama la mgawanyo wa ubunge linawatoa jasho je la Mgombea Urais litakuaje?? hili ni tatizo na wanatupeleka babaya kuanza kuhoji uhalali wa ndoa yao wakiwa mbele ya Tv na Camera wanaonekana wanapendana sana wakijua tunawatazama wakiwa nje ni sheedah kila mmoja anavutia kwake! je kweli hawa wanawatetea wananchi au wanamalengo mengi? Na je hi ndoa yao yenye mgogoro wa majimbo itakapofika zamu ya kumpata mgombea mmoja wa urais itakuaje???