Majimbo Sita yatakayoamua mshindi wa Urais Marekani!

jmushi1

Platinum Member
Joined
Nov 2, 2007
Posts
26,329
Reaction score
25,263
Wataalamu wanaamini kuwa kuna majimbo machache tu ambayo yanaweza kumuwezesha mgombea wa Democratic Kamala au mpinzani wake wa Republican, Donald Trump kushinda uchaguzi mkuu wa Marekani hapo November.

Sita kati ya majimbo hayo-Arizona, Georgia, Michigan, Nevada, Pennsylvania na Wisconsin - wagombea hao wanaonekana kuwa kwenye mchuano mkali, na pengine yanashikilia ufunguo wa nani ataingia Ikulu ya Marekani.

Hadi usawa huu mchuano ni mkali baina ya wagombea hao wawili.

Na hii ni kwa mujibu wa Foxnews ambao ni chombo cha habari kinachomsapoti Trump na Repunlicans kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Fox News, Harris na Trump wamefungana katika majimbo mawili (Michigan na Pennsylvania),

Trump yuko mbele kwa pointi 1 huko Wisconsin, na Harris yuko juu kwa 6 huko Minnesota.

Utafiti mpya unaonyesha kuwa Rais wa zamani Trump na Makamu wa Rais Kamala Harris wamelingana, licha ya rais huyo wa zamani kuongoza kwa karibu tarakimu mbili kipindi Biden akiwa mgombea.

Utafiti wa Detroit News WDIV-TV, uliofanywa baada ya Rais Biden kujiondoa katika kinyang'anyiro cha 2024, uligundua kuwa Trump na Harris wanalingana kwenye uungwaji mkono wa 41% huko Michigan, wakati 6% ya wapiga kura wa Michigan bado hawajaamua.

Matokeo ya kura yanaonyesha mabadiliko makubwa ya uungwaji mkono tangu uchunguzi wa Januari uliofichua kuwa Trump alikuwa akiongoza dhidi ya Biden katika jimbo hilo kwa alama 8.

Direct win for trump nchi kama marekani hawawezi kuongozwa na mwanamke hata kama wao ndio waasisi WA 50 Kwa 50.
 
Yaani kuufuatilia uchaguzi wa Marekani hadi raha maanake dunia nzima inasimama, huu ndio uchaguzi hakuna mizengwe wala hila kwa chama chochote wala mgombea yeyote, ni kama tu kufuatilia mashindano ya kombe la dunia.

Tofauti na wengine wanavyofikiri kwamba Marekani hawawezi kuwa na rais mwanamke mimi natofautiana nao. Marekani ni nchi ambayo watu wana upeo mpana sana wa kujua nini wanacho kihitaji na kwa wakati gani.

Wananchi wa Marekani baada ya kuongozwa na marais 46 wanaume sasa wanaona kuna haja ya kujiuliza ni kwa nini wasimjaribu na mwanamke pia safari hii.

Hii inadhihirishwa na namna uchaguzi uliopita ulivyokuwa mkali kati ya Bw. Donald Trump aliyeibuka mshindi na Mama Hillary Clinton hivyo basi safari hii chochote chaweza kutokea na kupelekea historia ya Marekani kuandikwa upya.

Wataalamu wanaamini kuwa kuna majimbo machache tu ambayo yanaweza kumuwezesha mgombea wa Democratic Kamala au mpinzani wake wa Republican, Donald Trump kushinda uchaguzi mkuu wa Marekani hapo November.

Sita kati ya majimbo hayo-Arizona, Georgia, Michigan, Nevada, Pennsylvania na Wisconsin - wagombea hao wanaonekana kuwa kwenye mchuano mkali, na pengine yanashikilia ufunguo wa nani ataingia Ikulu ya Marekani.

Hadi usawa huu mchuano ni mkali baina ya wagombea hao wawili.

Na hii ni kwa mujibu wa Foxnews ambao ni chombo cha habari kinachomsapoti Trump na Repunlicans kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Fox News, Harris na Trump wamefungana katika majimbo mawili (Michigan na Pennsylvania),

Trump yuko mbele kwa pointi 1 huko Wisconsin, na Harris yuko juu kwa 6 huko Minnesota.

Utafiti mpya unaonyesha kuwa Rais wa zamani Trump na Makamu wa Rais Kamala Harris wamelingana, licha ya rais huyo wa zamani kuongoza kwa karibu tarakimu mbili kipindi Biden akiwa mgombea.

Utafiti wa Detroit News WDIV-TV, uliofanywa baada ya Rais Biden kujiondoa katika kinyang'anyiro cha 2024, uligundua kuwa Trump na Harris wanalingana kwenye uungwaji mkono wa 41% huko Michigan, wakati 6% ya wapiga kura wa Michigan bado hawajaamua.

Matokeo ya kura yanaonyesha mabadiliko makubwa ya uungwaji mkono tangu uchunguzi wa Januari uliofichua kuwa Trump alikuwa akiongoza dhidi ya Biden katika jimbo hilo kwa alama 8.

Niamin.Trump anamzidi huyo Harris mbali sana.

Isipokua Media!!! media za Marekan. Wengi ni Pro Demos , kwahiyo kinachofanyika hapo ni kuhakikisha wanaonyesha kua Kamara anakubalika ili wahamishe mawazo ya Independents na Demos ambao walikua wameshaamua kumgeukia Trump.
 
Nimeweka link ya Fox News mkuu au haujacheki?
 
Back
Top Bottom