Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Wanamikakati ya CCM hawafikirii vizuri. Kitendo cha wao kusuka njama ili kuwaengua wapinzani kwenye majimbo ya ubunge na udiwani ni kitendo kitakochokwenda kumgharimu Magufuli kura za urais.
Wananchi wanatafsiri kuwa kuwanyima choice kwenye ubunge na udiwani kwa kuwalazimishia watu kushinda bila kupingwa ni dharau kwao, ni dhulma dhidi yao na ni kitendo cha kuwanyima haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba yetu ya nchi. Hasira hizi za wananchi zinakwenda kuelekezwa kwa raisi Magufuli kwa kumnyima kura, kwa mujibu wa falsafa ya kama unaninyima mboga basi na mimi Ugali sitoi!
Hii mbinu ya kuengua wapinzani ingewafaa CCM kama kungekuwa na mgombea dhaifu wa Upinzani au kama Upinzani ungekuwa dhaifu. Lakini Lissu ameamsha ari za wananchi, anawapa elimu ya uraia, anawapa hasira wananchi kwenye mikoa ambayo wagombea wengine wa ubunge na madiwani wameenguliwa, kwa hiyo wananchi wanatafsiri kuwa uonevu huu unasababishwa na Magufuli na kwa hiyo watapiga kura za kumkataa.
CCM kama wako Smart, wangeachana na hii biashara ya kukimbilia ushindi wa mezani kwenye ubunge maana itawagharimu sana kura za uraisi.
Logic iko Simple tu, Ukininyima kumchagua mbunge nimtakaye, au na madiwani ninaowataka basi hata huyo rais mnayeomba nimchague naye nitamkataa!.
Lissu ameamsha ari na hasira ya wananchi hasa kule kwenye majimbo ambayo wagombea wa upinzani wameenguliwa kibabe!