Mimi nina historia nzuri na BIBI AKIDA kupitia kwa ALLY wa LINDI MJINI ππΎπ
Charles...
Wanasema chini ya kila paa kuna historia.
Tuwekee historia hiyo.
Mimi nakuwekea hapo chini historia ya Ali Ibrahim Mnjawale:
''Tawi la Lindi lilikuwa tayari lina uhusiano na makao makuu ya TANU mjini Dar es Salaam, na lilikuwa likitarajia kuhudhuria mkutano huo na kukutana na Julius Nyerere na uongozi mzima wa TANU pale makao makuu Dar es Salaam.
Salum Mpunga, mwanachama muasisi wa TANU, na
Ali Ibrahim Mnjawale waliteuliwa kuhudhuria mkutano huo kama wajumbe kutoka Jimbo la Kusini.
Halmashauri ya TANU ya Lindi iliwaelekeza wajumbe hawa wafikishe ombi rasmi kwa makao makuu ili Julius Nyerere aje kufanya ziara kusini kwanza, kukutana na wananchi na kufanya kampeni kwa ajili ya TANU na pili aje kupambana na propaganda dhidi ya TANU zilizokuwa zikitawanywa na Yustino Mponda.
Mponda akitumia uhusiano wake na serikali ya kikoloni na nafasi yake kama mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria kutoka Newala; na vilevile akitumia ushirikiano wake wa muda mrefu na kanisa ambao bila shaka yoyote lilikuwa serikali ndani ya serikali kule kusini, alikuwa ameanza kampeni yake ya kuipinga TANU.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
Huu ulikuwa Mkutano Mkuu wa kwanza wa TANU uliofanyika Hindu Mandal Gandhi Hall, Dar es Salaam 1955.
Angalia picha hapo chini: