Majina ya mahali au sehemu mbalimbali za kufanyia shughuli mbalimbali

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Mahali mbalimbali

Kuna mahali au sehemu mbalimbali za kufanyia shughuli mbali mbali.
Yatazame maelezo ya mahali yafuatayo.
1. Maktaba: sehemu ya kuwekea vitabu kwa ajili ya kusoma na kuazima.

2. Makavazi: mahali ambapo vitu vya kale huwekwa kuchunguzwa na kuonyeshwa.

3. Maabara: sehemu ya kufanyia utafiti wa kisayansi.

4. Bohari: sehemu ya kuhifadhia silaha.

5. Karakana: mahali pa kutengenezea vitu kwa mitambo.

6. Hospitalini: sehemu ya kutolea matibabu kwa wagonjwa.

7. Ufuoni/makafani: Sehemu ya kuhifadhia maiti.

8. Pambajio: sehemu katika nyumba ambapo watu hukaa kungojea zamu zao.

9. Sebule: chumba cha kupokelea wageni na cha mazungumzo

10. Hamamuni: chumba cha kuogea.



11. Mahakamani: Mahali ambapo kesi husikilizwa na kuamuliwa.

12. Stanini: Mahali pa kuabiria na kushikia magari ya usafiri ya umma.

13. Kivukomilia: Mahali rasmi pa kuvukia barabarani palipochorwa mistari mieupe.

14. Maegesho: Mahali speshieli pa kuwekea/kuegesha magari.

15. Korokoroni: Chumba katika kituo cha polisi cha kuwafungia washukiwa.

16. Gerezani/Husuni: Sehemu ya kufungiwa wahalifu ili kuadhibiwa warekebishe mienendo yao.

17. Rumande: Chumba katika gereaza wanapofungiwa mahabusu wanaosubiri kumalizika kwa kesi zao.

18. Maabadini: Mahali a kuabudia.
19. Mskitini: maabadi ya waislamu.

20. Hekaluni: Maabadi ya wayahudi.
 
21. Sinagogi: maabadi ya Wayahudi.

22. Kanisa: maabadi ya Wakristo

23. Mahame: mahali palipohamwa (ganjo/tongo)

24. Kizimbani: sehemu ya mahakamani asimamapo mshtaki, mshtakiwa au shahidi wakati wa kesi.
25. Fuko: mahali kuku hutagia

26. Ghala/stoo: jengo la kuhifadhia bidhaa
27. Madobini fuo: mahali maalum ambapo madobi hufulia nguo

28. Chimbo: shimo kubwa ambapo huchimbuliwa udongo, mchanga au madini.

29. Mapokezi: ofisi ya kupokelea wageni
30. Kilinge: mahali pa uganga


ZOEZI Andika jibu mwafaka.
1. Chumba cha kufanyia utafiti wa kisayansi ni ____________.
2. Chumba cha wanafunzi cha kulia huitwa ______________.
3. Mahali pa kuokea vyungu huitwa ____________.
4. Sehemu ya kuhifadhi nafaka ni __________.
5. Nyumba ya kujilindia kutokana na adui huitwa _________
6. Ukumbi wa mazungumzo huitwa _________.
7. Mahali k.v meza pa kutolea huduma mbalimbali huitwa _________.
8. Mahali pa kushuka pwani kutoka melini huitwa ____________.
9. Mahali panapouzwa chai: kahawa na vyakula vingine huitwa___
10. Mahali pa kutengenezea vyombo vya usafiri huitwa _________


Andika jibu mwafaka.
11. Chumba cha kupigia na kurushia picha huitwaje? __________.
12. Wanyama hupelekwa __________ kula.
13. Mahali ambapo wanyama huchinjiwa huitwa _______________.
14. Sehemu ambapo mtu huenda haja ni ________________.
15. Mahali ambapo wavulana hutahiriwa huitwaje? ___________
16. Mahali panapouzwa chakula na vinywaji k.v katika shule huitwa ____________.
17. Duka la vipodozi na utengenezaji wa nywele huitwa _______________.
18. Mahali pa kuogeshea mifugo k.v. mbuzi na ng’ombe huitwaje? ______________.
19. Nyumba ya kulala wanafunzi katika shule au chuo huitwa _____________.
20. Mahali pa kupikia ni _______________.
 
Majibu tafadhali
 
1 Maabara
2 Bwalo
4 Ghala
5 Handaki
9 Mgahawa
12 Malishoni
14 Maliwato
18 Josho
19 Bweni
20Jikoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…