Majina ya marais wote wa Tanzania yana herufi M

mapipando

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
2,922
Reaction score
3,559
Wakuu habari zenu,

Kuanzia rais wa kwanza wa Tanzania hadi wa sasa katika majina yao iwe matatu au manne hakujawahi kukosekana jina linaloanzia na herufi M.
Mfano,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Alhaji Ally Hassan Mwinyi
Benjamin William Mkapa
Jakaya Mrisho Kikwete
Dr.John Pombe Joseph Magufuli

Je,kuna makusudi yeyote katika hiyo herufi au imekuwa ikitokea tu accidentally?
 
Kwenye jina la Nyerere hakuna M, hiyo mwalimu ni kwasababu ni mwalimu kitaaluma na sio jina lake
Jina lake halisi ni:- Julius Kambarage Nyerere. Nioneshe hiyo M hapo[emoji115] [emoji115]
 
Kwenye jina la Nyerere hakuna M, hiyo mwalimu ni kwasababu ni mwalimu kitaaluma na sio jina lake
Jina lake halisi ni:- Julius Kambarage Nyerere. Nioneshe hiyo M hapo[emoji115] [emoji115]
Uko sahihi,ila pamoja na hayo hilo jina la heshima limeanzia na M.
Kwahiyo kama kulikuwa na lengo basi limetimia pasipo kujali ni halisi ama la kutengeneza,I mean la heshima.
 
Uko sahihi,ila pamoja na hayo hilo jina la heshima limeanzia na M.
Kwahiyo kama kulikuwa na lengo basi limetimia pasipo kujali ni halisi ama la kutengeneza,I mean la heshima.
Kwanza hilo sio jina, ref katika types of names (nomino) hakuna kitu jina la heshima, hiyo ni kama hadhi tu. Sio jina
 
Mkuu usimnyime JK hadhi yake, anaitwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
 
Uko sahihi,ila pamoja na hayo hilo jina la heshima limeanzia na M.
Kwahiyo kama kulikuwa na lengo basi limetimia pasipo kujali ni halisi ama la kutengeneza,I mean la heshima.
Chief vp? Hivi unafeli wapi wakati mara nyingi hadhi ya mtu huoneshwa kwa ngeli ya A - WA au YU-A-WA.
Hilo sio jina bali ni hadhi tu, na hadhi nyingi ni lazima zianzie hivyo nenda kaangalie umoja na wingi wake ukoje.
Kasome kiswahili. Vile vile vitu vingi, miti, matunda, wanyama hapa duniani majina yake yameanzia na M. Hii mada isiwe ni chanzo cha kulink kujitokeza hizo M nyingi na Ufreemason.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…