Majina ya utani ya walimu

255Gene

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
888
Reaction score
1,090
Habari za saa hii wanajamvi..
Naimani wengi wetu tume kwenda shule na haka tabia pia kakubatiza walimu majina wengi wetu tulikuwa nako...

Nikianza na mimi Sec kulikuwa na Mwalimu wetu wa civics wakike alikuwa anapenda sana kutamka neno sovereignty hivyo tukaamua kumtungia hilo jina....

pia kulikuwa na huyo mama yeye alikuwa anavaa skirt ya ya kawaida na mshati mkubwa tukamtungia jina Bibi...

teacher wetu mwingine wa kiume alikuwa anafundisha physics alikuwa anabonge la kipara tuakambatiza jina kiparaa(kwa lafudhi ya ki arusha zaid)..

mwingine wa kiume tulimbatiza uwa uwa maana yeye alikuwa
akikushika akuchape alikuwa anachapa haswa.


karibu tujikumbushe majina ya utani ya walmu wetu.
 
Sisi mwalimu wetu mmoja alikuwa anachapa balaa...tulikuwa tunamuita Bwana Pepsi... usithubutu kukutwa na Bwana pepsi, ukisikia hivyo unakuwa makini mno
 
sisi mwalim alikuwa na kipara tukamuit mwampara
 
Mmoja alikuwa na Madevu sana tukamwita SAVIMBI, hiyo ilikuwa Tambaza ya enzi hizo
 
Jamaa tcha alikuw anatufundsha physics "relative density " ilichukua mda mrefu xana hyo maada mpka jina lake tukamwita DENSITY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…