Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 19,484
- 38,416
Kwa takribani siku tatu tumesikia kuwa kuna Viongozi wa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na CCM wanaomiliki akaunti huko nchini Uswisi. Mambo hayo nakumbuka miaka ya nyuma tulikuwa tukisimuliwa alikuwa akiyafanya Marehemu Mobutu Seseseko wa Zaire. Tunaomba yeyote anayejua majina ya Vigogo hao wanaotuibia kupitia makampuni yaliyowekeza kwenye madini, mafuta na gesi aweke majina yao hapa.