Majina ya vinywaji vyetu vya asili

We ngalikihinja mwana wa yani? ummanyile na msongela? ah pale namatuhi ndo pa bomani bwana, ummanyile na mbema?

Kwa wasiojua 'kiingereza'😀!

"Wewe Ngalikihinja ni mtoto wa nani (ni ukoo gani)? Unamfahamu hata Msongela! Pale Namatuhi ndio kwetu bwana, unamfahamu na Mbema?"
 
Kwa wasiojua 'kiingereza'😀!

"Wewe Ngalikihinja ni mtoto wa nani (ni ukoo gani)? Unamfahamu hata Msongela! Pale Namatuhi ndio kwetu bwana, unamfahamu na Mbema?"

Dah kaka smu wewe kiboko, kweli ki english wakijua hahaha dah kweli nimefurahi mno!
 


Yaani pale pale mfaranyaki bwana, bombi ii nyumbi ii, halafu ukienda Magagula unapata Myakaya kwa sana, Yaani umenikumbushi home bana
 
Yaani pale pale mfaranyaki bwana, bombi ii nyumbi ii, halafu ukienda Magagula unapata Myakaya kwa sana, Yaani umenikumbushi home bana

Mkuu kunyumba kuzuri sana, wakati huo no tv, jioni tunashinda kwenye ngoma, mitaa ya mateka, makambi, kimolo, matogoro na kule luhila, mkuu asikwambie mtu kuna ngoma hiyo inaitwa kambindi, wacha bana, ikifika kuanzia mwezi wa sita komunio ya kwanza na vipaimara sherehe kila nyumba hahaa acha mkuu kitoweo mkuu wa meza.
 
Rubisi--hii inapatikana Bukoba; inatengenezwa kutokana na ndizi
Mnanasi --Hii nayo ni Bukoba inatengezwa kutokana na nanasi
Mapuya--Hii inapatikaka Usukumani
Kangala--Inapatikana Usukumani
Chitukuku--Sengerema/Geita
 
PINGU nasikia pombe hii mnywaji akianza kulewa muuzaji wa pombe huwa na kamba tayari kumfunga nayo miguu (suruali) ili asichafue mazingira.
 
Lemomo - inatengenezwa na malimao asili yake siijui
Manguree - hii nadhani kwa wale wasandawe watatusaidia recipes
 
Comoni inapatikana iringa inatokana na vimelea vya mahindi
kangala-Iringa inatokana na pumba za mahindi
Msabe- Iringa,inatokana na mtama
Sweera-Iringa inatokana na vimelea vya mahindi pamoja na asali
Pia kuna kihambule, hii inatengenezwa kwa vimelea vya mahindi
 
ulevi.......ulevi....ulevi.......jamani
 
how can i get one? mbege... how is it? strong? I need something light...🙂
 
poleni sana huku village kuna pombe inaitwa kanyeto basi ukinywa inashuka down,from mpang'anyang'nya village
Conquest
 
pingu mbona hamjaitaja???
nasikia hiyo ukinywa lazima uendeshe na breki zote zinagoma kabisa.
inabidi mama muuza akufunge pingu miguuni ili usijekumchafulia mazingira.
kazi kwa wake za wanywa pingu..sipati picha.
 

Mkuu hizi power no. 1 za malawi tunabugia hapa Mbeya Kumbe ni gongo? hakianani!! Kumbe Tunapiga gongo bila kujua!! Mungu wangu!!!
 
Sasa mungu amekukosea nini mpaka umlilie hivyo..Nafsi yako ndo ya kuililia kwa kupenda kupata stimu mapema ya machozi ya kenge!!...Ila kwa mikoa kama mbeya na iringa vinywaji vikali ndo vinawafaa kupunguza makali ya baridaaa
 
GONGO, chang'aa, Piwa,
wanakunywa kama wewe unavyokunywa bia.

Mkuu kimsingi gongo (au chang'aa, piwa, machozi ya simba) sio pombe ya asili kwetu. Gongo ni pombe ya mvuke (spirit) na sidhani kama kuna kabila (hapa Tanzania) lenye asili ya kutengeneza hizi pombe za mvuke!
Pombe za kiasili (au kienyeji) zinatokana na mazao (yenye wanga/sukari) yanayopatikana mahali husika.
Swali langu ni Je, wamasai (na makabila ya wafugaji) wana pombe za kienyeji/asili? Gongo hapana hii asili yake si umasaini, japo inatumika sana kwa wamasai.
 
Gwaga - Made in Ngara by Wahangaza, it's an equivalent of Haya's rubisi ila kule hawatengenezi kwa miguu..ikigundulika umetumia miguu.....utainywa mwenyewe..nobody will buy it either. But there is also Umusharuro and Impeke! the latter being the best than the former made in mtama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…