Majina ya Wakenya



Mkishakuwa nchi moja yenye makabila tofauti na kila kabila likawa too proud na utamaduni wake basi lazima kutakuwa na migawanyiko ambayo huzua chuki na vurugu ambazo wanasiasa na hata mataifa ya kigeni huzitumia kwa faida yao,

Kuondoa hali hiyo inabidi kujenga tu nchi yenye utamaduni mmoja ikiwemo lugha moja

Kiswahili kinaongelewa na wananchi karibu wote na pia kina maneno mengi yenye asili ya makabila ya Kenya, Congo, Tanzania n.k so sio mbaya ikachukuliwa kama lugha ya asili kuliko ya kigeni.

Ingekuwa jambo zuri kama ukanda wa Afrika mashariki na kati tungekuwa na lugha moja iliyoundwa kutoka lugha za makabila ya nchi zetu, bahati mbaya kila mtu yupo too proud
 

Lugha ya Kiswahili tunaipenda na inatuunganisha baina ya makabila, ila siwezi kuacha kuongea na mtu wa asili yangu kwa lugha yangu ya asili nihamie kwa Kiswahili, huo ndio tunaita utumwa.
 
Lugha ya Kiswahili tunaipenda na inatuunganisha baina ya makabila, ila siwezi kuacha kuongea na mtu wa asili yangu kwa lugha yangu ya asili nihamie kwa Kiswahili, huo ndio tunaita utumwa.
Nd ndio tatizo nililolisema, hakuna mtu aliyetayari ku sacrifice cha kwake kwa ajili ya kupata cha wote, mgawanyiko utaendelea kuwepo
 
Sio la kutoka kwa lugha zetu asili hilo ni la sheng za Mombasani. Linamaanisha mtu wa madili na pesa za fasta fasta. Ila hata jina langu halisi sio la 'kizungu' hata kidogo. Jina 'kali' sana la kiafrika. Kama la wameru, sampuli za kina Gitobu Imanyara, Mwenda M'Mbijiwe, Kinoti M'Mtoaboo na wengine kama hao. 😄
 
Mkuu pingli-nywee jina lako lina maana gani?
 
kwa taarifa Yako Kuna majina mengi wanayoshare wakalenjin na wakikuyu kama Maina, Kimaru, Mutai, Kirui
 
kwa taarifa Yako Kuna majina mengi wanayoshare wakalenjin na wakikuyu kama Maina, Kimaru, Mutai, Kirui
Kumbe..mixed marriage sio? I hope itaongezeka zaidi, mwisho kusiwepo na jina linaloweza kuwa associated na kabila fulani, ndio taifa linavyojengwa
 
Nd ndio tatizo nililolisema, hakuna mtu aliyetayari ku sacrifice cha kwake kwa ajili ya kupata cha wote, mgawanyiko utaendelea kuwepo

Kutumia lugha sio sacrifice, ni mfumo wa kuwasiliana, leo Mfaransa aache kuongea Kifaransa na Mfaransa mwenzake waongee Kingereza eti ndio sacrifice.
Nikiwa na ndugu wangu wa asili anayeongea lugha yangu ya asili, hatutahamia kwa lugha ya kuja na kutelekeza asili yetu, ila nikikumbana na asiye wa asili yangu tutahamia kwa lugha inayotuunganisha, kwa mfano nikiwa Sudan pale hivi majuzi nilikua natumia Kingereza muda wote kwa Waafrika wenzangu maana ndicho kilikua kinatuunganisha, hapo Kiswahili au lugha yangu ya asili haikua na umuhimu wowote.
 
Unachanganya mambo hapa, Ufaransa ni taifa sio kabila ndani ya taifa, so wakiwa na lugha moja ndivyo inavyotakiwa.

Na hisia za namna hii kujiona kabila ni kama taifa ndio ujinga wa makabila
Matatizo ya huko South Sudan ndio yanatokana na hizi akili, watu ndani ya taifa moja wanajiona tofauti wakati wanafanana karibu kila kitu, mambo mengi, wanapigana kama wanyama na kutegemea misaada ya wazungu
 
Raila
Wafula Chebukati
andika vizuri majina ya watu.
 
Ya kimagharibi hayaleti udini?!
 

Siongei kuhusu taifa, naongea kuhusu asilia ya binadamu, haya mavitu mnaita mataifa yamebuniwa na wazungu, wamekuja na kuchora chora mipaka yao na kuagiza watu waache asilia zao waingie kwenye huo utumwa. Unakuta Mmaasai hapo mpakani umemchorea mpaka na kumuambia ajiite Mtanzania na ndugu yake upande wa pili ajiite Mkenya kisha unawaambia waache kutumia lugha yao ya asili baina yao waongee hicho Kiswahili ambacho hata chenyewe sio lugha ya asili, isingekua kwa jitihada za mwarabu kubaka wazee wetu Pwani hakingebuniwa.

Umuhimu wa lugha ni kuwasiliana, basi, ikitokea hauongei lugha yangu ya asili basi itabidi tuhamie kwenye lugha itakayotuwezesha kuwasiliana, tutahamia kwenda kwenye Kiswahili, kikishindikana twende kwenye kingereza n.k.
 
Mkiwa ndani ya mipaka na mnaongozwa na serikali fulani tayari ni taifa, liwe limewekwa na wazungu ama la tayari ni taifa

Taifa linatakiwa kuwa cohesive kwa ajili ya stability, ama mtakua mnapigana kama koo za nyani msituni
 
Mkiwa ndani ya mipaka na mnaongozwa na serikali fulani tayari ni taifa, liwe limewekwa na wazungu ama la tayari ni taifa

Taifa linatakiwa kuwa cohesive kwa ajili ya stability, ama mtakua mnapigana kama koo za nyani msituni

Watu kuwa kimoja inategemea mambo mengi sana, Somalia kule huongea lugha moja wote, tena dini moja ila miaka yote mavita vita hawaijui amani.
Kwa taifa kuwa na utengamano kunategemea mambo mengi yakiwemo haki za kidemokrasia na kisheria.
Watu wanaweza wakaishi pamoja huku wakienzi tamaduni zao na asilia zao, ila wakawa kimoja kwenye mambo ya utaifa.
Au wachague kuswagwa kama mifugo kwenye lugha moja, mtazamo mmoja na kusidinkwa humo humo ndani kiasi kwamba hata uongozi unabaki wa chama kimoja miaka yote.
 
Somalia kuna makabila na koo nyingi ndio chanzo cha ugomvi wao
Somalia, Ethiopia, Sudan, DRC., Kenya etc maugomvi yao ni kutokana na kuendekeza huu ujinga wa makabila
 
Somalia kuna makabila na koo nyingi ndio chanzo cha ugomvi wao
Somalia, Ethiopia, Sudan, DRC., Kenya etc maugomvi yao ni kutokana na kuendekeza huu ujinga wa makabila

Somalia wanaongea lugha moja, dini moja na ni mfano hai wa namna lugha haitoshi kuondoa ujinga, mnaweza mkaongea lugha moja lakini mpo mazombi tu miaka yote hamueleweki mnakotoka na mnakokwenda.
 

Wabongo wasioweza kuunda hata sentensi moja kwa Kingereza wanaitwa John Peter Michael au Abdallah Hussein Ally. Tena sasa wanashindana kuwapa watoto majina ya ajabu ajabu unakuta mtoto mweusi na kipilipili kichwani anaitwa Cookie. Ni fedheha hawa wamatumbi.
 
[emoji23][emoji23] kwema mkuu ? Mkenya pekee unayeongea kiswahili fasaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…