Majina ya wakurya na maana zake

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Majina ya kwanza kwa watoto wa kwanza wa kiume

Marwa-Pombe
Mwita-vita
Chacha-zimekuja( ng'ombe zilizoibwa zimekuja)

Majina ya kwanza kwa watoto wa kwanza wa kike

Rhobi- msururu wa( hasa ng'ombe wengi wakiwa wanatembea kwa mstari mmoja)
Ghati- uzao( au mungu wa kuumba watu)
Bhoke- asali

Majina mengineyo ya kawaida

Wambura- mvua
Wankuru-kobe
Matiko/matiku-usiku
Mbusiro- mbegu
Wankyo-Asubuhi
Magoiga- aina ya nyoka
Nyamhanga- aina ya mnyama mdogo jamii ya sungura
Nyamugi-mji
Magesa-mavuno
Nyerere-aina ya wadudu jamii ya vipepeo ambao hudondoka na kuanza kushambulia mazao au mimie
Matinde-mabonge ya udongo yaliyolimwa shambani hayajalainika
Nyaigana- shilingi mia moja
Wanchara-njaa
Kerombe-nyasi ndefu hasa maeneo ya pori
Wangubo-kiboko
Sensema-kimbia mdogo mdogo
Mang'iti-fisi
Waitara-ghala la kutunzia chakula
Mhindi- mhindi nafaka
Nyangi-harusi
Gesaku-Mlango
Nyangwine-mamba
Itembe-nyumba ya tembe
Koroso-moto wa kuota jioni hasa wazee na vijana wa kiume
Maginga-eneo lililotengwa kwa ajili ya malisho ya ng'ombe au kwa ajili ya kukata nyasi au eneo liloachwa baada ya kulima

Majina ni mengi endelea kuchangia majina mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…