Ni ufisadi tu unaozuia.
Kama mnavyojua kuna shule nyingi za binafsi zinamilikiwa na vigogo; walichofanya ni kuchelewesha kutoa selection ili kwanza shule zao zijae. Si unajua kama wewe ni mzazi una mtoto amemaliza kidato cha nne unakuwa huna uhakika atapangwa shule gani, na kadri muda unavyokwenda na shule binafsi kuzidi kujitangaza na kuanza masomo, unafika wakati unasema ngoja nimpeleke private nisije kukuta hakuchaguliwa huko serikalini au kachaguliwa shule isiyo nzuri. Akifika huko ni kulipa kwanza nusu ya karo ya mwaka. Ina maana hata ukikuta kachaguliwa shule nzuri ya serikali utashindwa kumhamisha kwani utakuwa umelipa pesa nyingi tayari, na hata ukimhamisha mwenye shule tayari kaingiza kipato.
With computerisation selection haiwezi kuchukua zaidi ya wiki 3 even less. Nafasi zilizopo zinajulikana tena kwa comb zake, si unaset formula tu na inakupatia selection! tena kwenye excel tu.