Majina ya wauza Mihadarati Tanzania/Kenya (Kifo cha George Saitoti).

Majina ya wauza Mihadarati Tanzania/Kenya (Kifo cha George Saitoti).

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Posts
11,584
Reaction score
6,136
Nimeangalia video ya Jicho Pevu (Jicho Pevu: Ghururi ya Saitoti - Uchunguzi wa kifo cha Saitoti) inayorushwa na KTN Kenya.

Ukiiangalia na ukalinganisha na yanayojiri Tanzania, kuna mambo mengi sana yanafanana. Ila inabidi nikubali kuwa Wakenya wako juu sana kwa mambo mengi na hata u-MAFIA wao kwa kweli ni wa hali ya juu. Vifo tata ambavyo vipo wazi kabisa, Usalama wa Taifa wa Kenya wamefanya ubavu wa hali ya juu ili kuficha ukweli wenyewe na kila mtu unaona kabisa anasita kusema.

Hapo ndipo unapoona faida ya kuwa na Wageni nchini kwa sababu maovu mengi wanafanya wao na mambo yakiharibika, basi jamaa wanafukuzwa nchini. Huwezi kuamini ndugu wawili wa Armenia, wanapewa vyeo vya juu vya POLISI na wanakuwa hawaguswi na hakuna mtu anaachishwa kazi. Kibaya zaidi ni kuwa Maboss wa Polisi na Usalama wa Taifa wanajua kila linalotendeka.

Ila nampa hongera nyingi Mohammed Ali na wenzake wote kwa ujasiri na utafiti wa hali ya juu walioufanya ingawa mwisho waligonga mwamba. Ukiangalia uchunguzi wao, unaona kabisa George Saitoti aliuawa kwa sumu na uchunguzi ukaharibiwa. Na kibaya zaidi ni kuwa REPORT ambayo ilikuwa itaje majina hayo ya wauza Midaharati, HAIJASOMWA.

Ukilinganisha tukio hilo, hivi kuna uwezekano ndiyo maana na Mheshimiwa Rais wetu wa Tanzania (kama Taasisi) na yeye ameshindwa kusoma majina hayo kwa woga wa kupatwa yaliyompata George Saitoti? Hivi kuna uwezekano kuwa nchi zetu tayari zinatawaliwa na kuongozwa na watu wa mataifa mengine? Au ni kuwa wameshika siri mbaya sana ambayo Serikali haiwezi kabisa kuwagusa?

Inasikitisha sana hapa tulipofika. Na kama ni kweli hawa jamaa wa ASIA na Eastern Europe wameshajiingiza sana kwenye nchi zetu na hivyo kuzitumia kwenye kusafirisha madawa hayo, basi inabidi tuombe msaada wa nchi za USA na EU. Sijui kwa Kenya sasa hivi hali ikoje na hasa baada ya kuingia Rais mwingine ingawa ukichunguza, unaona ni ndugu walewale.

 
Last edited by a moderator:
Hawa wafanya biashara wanavyo ogopwa ndivyo wanavyozidi kupata kichwa cha kuendelea kufanya hiyo biashara yao haramu. Na haya yanatokana baadhi ya wafanya biashara kua katika mifumo nyeti katika serikali
 
Kijana nilikuwa simfahamu ila kwa kweli nimemvulia kofia. Jerry Muro wetu wa TBC wakamzima pamoja na Mwanahalisi. Ila Mungu bariki bado wako hai maana ingelikuwa ni Kenya, wangelikuwa wameshazikwa siku nyingi.
Jamandaria la ujambazi na mohamed ali wa KTNTV.
 
Back
Top Bottom