Mzimu uko sahihi kabisa. Jina ni utambulisho kamili wa mtu. Kwa hiyo kama utambulisho wako unakamilishwa na maneno ishirini basi maneno hayo ishirini ndiyo jina lako. Mfano Waziri Mkuu wa Tanzania jina lake ni: Mizengo Kayanza Peter Pinda na aliyekuwa Raisi wa Zaire Kabla ya Lawrence Kabila jina lake ni Mobutu Seseseko Kuku Ngbendu Wazabanga.
Nawaomba waandishi wa vyombo mbalimbali wawe macho na wawasahihishe wateja wao pindi wakoseapo kiswahili. Wasiwaache wakosee na waondoke bila kurekebishwa. Wenzetu wa Rwanda wametunga sheria inayomtia hatiani yeyote anayepotosha Kinywarwanda. Sisi hatuna sheria sawia ya kulinda Kiswahili japo tunavyo vyombo lukuki visivyokuwa na meno.
Halafu mwingine anasema "sefuria lipo kwa jiko" na ni mswahili naye.
BAKITA, hivi kwanini mmelala hivyo. Kiswahili kinachafuliwa sana. Kiswahili fasaha ni Jina lako nani?. Sio Majina yako nani?.
Ukiulizwa jina lako nani, hapo utayataja yote hatakama yanafika kumi. Unamkuta kiongozi mkubwa tu wa Serekalini anasema, kwa majina naitwa Tumaini Kazinyingi, kwa Mfano. Wakati hicho sio kiswahili fasaha. Angesema tu Jina langu naitwa Tumaini Kazinyingi.
BAKITA mnafanya kazi gani?
Mkuu upo sahihi katika Kiswahili. Lakini usiwalaumu sana BAKITA kwa hapo ulipogundua japo kuna mengine isiwe sababu ya kuwalaumu. Binafsi nawafuatilia BAKITA na wanajitahidi sana kurekebisha pale ambapo wanaona kuna makosa.
Mkuu BAKITA ni BARAZA LA KISWAHILI TANZANIA. Sasa uwepo wao unamaana gani?
Hihihihahhahahaa! Ni hatari Mkuu. Yaani wale wasio jua kiswahili ndio wamekua watangazaji wa redio na Televisheni na Washereheshaji kwenye Masherehe.
Na watu wengine wanataka waongee kama mtangazaji Fulani.