Majina yetu na maana zake Kilatini

Unanikumbusha enzi naanza kujifunza Latin miaka ya 1991 nilipokua form 1 St.Peters Seminary.... Tulianza kwa kukariri sala ya Baba Yetu "Pater Noster Qui es ..."
 
MAANA YA MAJINA AMBAYO YANAPATIKANA KWEYE BIBLIA.

Na Darkgift

Amosi = Aliyesumbuliwa. Mbeba mzigo. Mwenye nguvu.
Andrea = Mwanamume.
Augusto = Anayestahili sifa
Ayubu = Mwenyekutubu
Barnaba = Kijana wa faraja
Benyamini = Mwana wa furaha (yaani mwana wa mkono wa kulia)
Danieli = MUNGU ni hakimu wangu
Daudi = Anayependwa
Debora = Nyuki.
Delila = Anayependa kujipendekeza.
Elizabeth. = MUNGU wa kiapo. MUNGU ni kiapo
Elisha = MUNGU ni wokovu
Eliya = YEHOVA ni MUNGU
Erasto = Anayependwa
Esta = Nyota.
Ezekieli = MUNGU ni mwenye nguvu. MUNGU anatia nguvu
Farao = Nyumba kubwa
Festo = Mwenye sherehe
Filemoni = Mwenye upendo. Mkarimu
Filipo = Rafiki wa farasi. Anayependa Farasi
Gabrieli = Mtu wa MUNGU
Gamalieli = Zawadi ya MUNGU. MUNGU anatoa thawabu
Gideoni = Anayepiga hadi kufa.
Haruni = Aliyeangaza. Anayeangaa
Hawa = Uhai.
Henoko = Kuweka wakfu
Hezekia = MUNGU ni nguvu yangu
Hosea = Wokovu.
Ibrahimu = Baba wa wengi
Imanueli = MUNGU pamoja nasi
Isakari = Yeye anatoa ajira. Ananipa mshahara
Isaya = YAHWEH anaokoa. YAHWEH ni wokovu
Ishmaeli = MUNGU anasikia maombi
Israeli = MUNGU anapigana. Anapigana na MUNGU
Karmeli = Bustani (ya MUNGU)
Kornelio = Mwenye pembe
Lawi = Umoja. Nia moja
Lazaro = Eleasar = MUNGU ni msaada. MUNGU amesaidia
Lea = Aliyechoka. Mwenye nguvu. Malkia wa nyumba
Luka = Mwanga. Kuangaza
Lutu = Shera. Pazia
Magdalene = Anayetoka Magdala
Malaki = Malaika wangu. Mpeleka ujumbe
Manase = Yeye (MUNGU) amenifanya kusahau
Martha = Malkia
Mathayo = Zawadi ya YEHOVA
Melkizedeki = Mfalme wa busara, Mfalme wa Amani.
Mika, Mikaya = Nani kama YEHOVA
Mikaeli = Nani anayelingana na YEHOVA
Moleki = Mfalme
Musa = Anayevutwa juu
Naftali = Mapambano. Vita vyangu
Naomi = Uzuri wangu. Anayenipendeza. Mzuri
Nathanaeli = MUNGU ametoa
Nathani = Yeye (MUNGU) ametoa
Nehemia = YEHOVA anafariji
Nikodemo = Mshindi wa taifa
Nuhu = Mapumziko
Obadia = Mtumishi wa YEHOVA
Onesimo = Mwenye faida. Anayesababisha baraka
Penina = Ushanga
Penueli = Uso wa MUNGU
Petro = Jiwe. Mwamba
Pilato = Aliyejiandaa kwa mkuki
Potifa = Mkuu wa walinzi
Prisila = Priska mdogo
Priska = Mzee. Anayestahili heshima
Rabi = Bwana wangu
Raboni = Bwana wangu (mkuu kuzidi Rabi)
Rahabu = Paana
Raheli = Kondoo jike
Rebeka = Mtego. Anayejipendekeza
Reubeni = Yeye (BWANA) ameona unyonge wangu. Angalieni
Rumi = Mji wa vilima saba
Ruthu = Urafiki
Safira = Mzuri. Anayependeza
Samsoni = Mwenye nguvu. Mwenye mwanga
Samweli = Aliyesikilizwa na MUNGU.
Vashti = (Mwanamke) mzuri
Sara = Anayetawala. Malkia
Saai = Ukoo wa kifalme
Sauli = Aliyeombwa
Sefania = YEHOVA anaficha. YEHOVA ameficha
Sefari = Anaunguza. Juu. Aliyeinuliwa
Sethi = Aliyewekwa sehemu ya pili. Kulipizwa
Simeoni = Kusikiliza maombi
Simoni = Kusikiliza maombi
Sinai = Kichaka chenye miiba
Sipora = Ndege (mdogo)
Stefana = Aliyevikwa taji.
Stefano = Taji
Sulemani = Mpole
Tabitha = Swala
Tera = Swala wa mlimani
Theofilo = Rafiki ya MUNGU
Timayo = Aliyeheshimiwa. Mwenye heshima
Timotheo = Anayeheshimu MUNGU
Tiro = Mwamba
Tobia = YEHOVA ni mzuri
Tomaso = Pacha
Trofimo = Anayekuzwa
Waebrania = Wanatoka pande zingine. Wavuka mpaka. Wageni
 
Jina langu latoka huko kwa Hitler.
Limegawanyika sehem mbili...
1. Means - Advice
2. Protection
Jina moja lenye kiima na kiarifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…