Majizo, Kusaga na Regina watumie njia gani nyingine ili wamuangushe Diamond na kundi lake? Kwanini wanashindwa? Tuwasaidie

Umaarufu alioupata Dai kipindi kile umemsaidia aendelee ila hakuna atakaempeleka mbele kinidhamu kimafanikio na kiubunifu zaidi ya hapo alipofika.
Endelea kupiga ramli tu lkn jamaa anazidi kujenga CV,mpaka sasa ana show 30 booked,jana katangaza show Ethiopia,mwezi ujao Malawi,ana show Madagascar miji mitatu,ana show za One Africa (Dubai,New York na London),bado hapo anashow za Wasafi festival Wadhamini wa kumwaga,juzi South Africa album yake ya A boy from Tandale imechukua tuzo.

Manake mnasema Youtube ananunua views lkn boomplay upande wa Tanzania anakimbiza miezi miwili wa 4 na watano (Refer Boomplay insta account).

Alafu mbona kuna wasanii kibao walikuwa maarufu huko nyuma,lkn hata show hawapati pamoja na kutoa nyimbo.
 
Diamond hawezi kufa kwa kuwa Kuna team Mond hao ni die hard fans. .ni kama Simba na Yanga..Msondo na Sikinde. .ndio maana ngumu msanii mpya kutamba. .Kuna manyumbu yameshajitune
 
Hakuna atakaempeleka mbele zaidi kinidhamu, kimafanikio na kiubunifu
 
Takwimu zinaonesha kwa Afrika Mashariki. Tz tunaongoza kwa imani za kishirikina. Si ajabu humu jf kuwa wachawi nguli.

Maana wivu wa kipumbavu ni sifa kongwe ya mchawi.
 
Sasa hao wengine wanao wapigia nyimbo zao kila siku mbona hawawafiki wakina DIAMOND na kumzidi?
Subiri yule dogo

Akiyeimba wimbo wenye maneno

Akipita minyama tu
akipita minyama tu

Atakuwa msanii mkubwa zaidi ya Jigga
 
Kwa hiyo hapo sasa nafsi yako imepata tulizo baada ya Diamond kushuka ?
 
Hakuna atakaempeleka mbele zaidi kinidhamu, kimafanikio na kiubunifu
Angekuwa hana nidhamu na ubunifu asingefika pale na bado anaisimamisha WCB kama kampuni,si swala dogo ndani ya WASAFI kuna Wasafi media,Wasafi Label na Wasafi Festival so bila kuwa na nidhamu na ubunifu leo hii asingeweza kumiliki vitu hivyo.
 
Youtube,insta et al,bado unategemea radio imuinue ama kumuangusha mtu ?Hiyo ilikuwa kabla ya 2014 Kabla mchina hajaleta smartphones
Hao walioenda kupiga magoti Clouds unadhan hawajui Kuna YouTube na Insta au kwa nini Diamond kaanzisha Radio station wakati YouTube ndo inatake over
 
Angekuwa hana nidhamu na ubunifu asingefika pale na bado anaisimamisha WCB kama kampuni,si swala dogo ndani ya WASAFI kuna Wasafi media,Wasafi Label na Wasafi Festival so bila kuwa na nidhamu na ubunifu leo hii asingeweza kumiliki vitu hivyo.
Muulize wasanii wangapi wenye majina makubwa wenye projects kubwa au zaidi ya hizo za Diamond?
 
Hao walioenda kupiga magoti Clouds unadhan hawajui Kuna YouTube na Insta au kwa nini Diamond kaanzisha Radio station wakati YouTube ndo inatake over
Kutokujiamini ni ugonjwa wa watanzania wengi wakiwemo hao waliokwenda kupiga magoti.
 
Angekuwa hana nidhamu na ubunifu asingefika pale na bado anaisimamisha WCB kama kampuni,si swala dogo ndani ya WASAFI kuna Wasafi media,Wasafi Label na Wasafi Festival so bila kuwa na nidhamu na ubunifu leo hii asingeweza kumiliki vitu hivyo.
Nidhamu aliokua nayo na ubunifu aliokuwa anapewa ndio imemsaidia hayo mafanikio zaidi ya hapo hatakua na zaidi
 
Damn..what a question!!
Hao walioenda kupiga magoti Clouds unadhan hawajui Kuna YouTube na Insta au kwa nini Diamond kaanzisha Radio station wakati YouTube ndo inatake over
 
Vituo binafsi vya watu kutopiga nyimbo za msanii ni adhabu?
 
Na kwa sasa hatutaweza pata mtu aliewaunganisha wasanii wakawa wanasikika karibia wote na kutoboa kimafanikio kama wakati Ruge yupo ulikua unaweza msikia Mwasiti katoa wimbo, Chege katoa wimbo, Shilole, Ney wa mitego na zikawa zote zinafanya vizuri na kualikwa kufanya show kila mahali lakin wakati huu watasikia wcb tu hata watoe mabata madogo hutaweza sikia wimbo unahit zaid yao ndipo tunasema bongo music inapotea
 
ukifattilia chanzo cha ugomvi utagundua kuwa hizo media zilitaka Diamond aperfom bure bila malipo kwenye matamasha yao ila jamaa akavunga sababu ya kujitambua yeye ni nani kwenye game, na wao wanajitetea kuwa wamechangia kumkuza kwenye muziki hivyo wana haki zote za kumpigisha shows bure eti dah! wengine wanaenda mbali zaidi kwa kusema "Ataona" >> source planet bongo dulla na jr. Dunia ya sasa imebadilika mnoooo watu hawasubiri kutoka kwa media wanatoka kwenye digital platforms na sosho mediaaaaa!!! Alafu akishakufa watakuwa wa kwanza kutangaza kifo chake kinafiki na kucheza nyimbo zake ilhali ameshafumba macho na hasikii masikiniiii!
 
Diamond alinitoka siku ile aliokuwa akimsalimia dingi wake studio, yaani mzee kajishusha lakini dogo hata heshima imemruka.

Ndukiiiii πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ

Utakuwa Mke wake Alikiba ww sio bure...hiyo chuki sio ya ya Kitanzania kabsaaa.
 
Kwa mwanaume aliekamilika hawezi akamwombea mwanamme mwenzake anguko.

Na wasiwasi na Jinsia yako mkuu, hizi tabia wanazo wanawake wa buguruni.

Pole sana.
Hujaelewa kabisa...jamaa anamsifia mondi na kuwacheka hao wanaotaka kumuangusha..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…