Majizzo: Nimeumia sana Hayati Rais Magufuli alikubali kuja kuzindua jengo letu la Efm

Majizzo: Nimeumia sana Hayati Rais Magufuli alikubali kuja kuzindua jengo letu la Efm

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Kupitia ukurasa wa Instagram wa mkurugenzi wa kituo cha habari cha Efm na TVE, Mbwana Francis Ciza alimaarufu Majizzo ameeleza namna alivyokamilisha taratibu zote za hayati Magufuli kuja kulizindua jengo lao la kituo hicho cha habari, Majizzo ameeleza kuwa –

Screen-Shot-2021-03-27-at-13.15.40.png


“Moyo wangu umejawa na maumivu makali. Mwanzoni mwa mwezi huu wa tatu, tuliratajia ujio wa aliyekuwa Rais wetu, Dkt #Magufuliwetu pale #EFMnaTve. Katika udogo wetu huu, udogo wa project yetu hii, tena tukiwa taasisi binafsi inayomilikiwa na Vijana, Hayati Magufuli alikubali kuja ofisini kwetu kufanya uzinduzi rasmi wa jengo letu. Taratibu zote za Kiserikali zilishaakamilika, alishatuambia anakuja. Tulijipanga kikamilifu (tafuta hashtag #WaswahiliKidedea, ambayo walipost rafiki zetu mbalimbali, hiyo ilikuwa tunaanza promo. Kuna wimbo mzuri wa Singeli tulishaautengeneza kwa ajili yake, tutautoa) ilikuwa tufanye tukio kubwa sana pamoja na Rais wetu kwenye ofisi zetu.

Can you imagine what i am feeling right now?, Pain. Nimeumia sana. Mzee huyu alituheshimu, alitaka kutuheshimisha zaidi, angekuja pale kuna milango mingi sana ingefunguka kwa ajili ya vijana wetu wa Uswahilini.
.
Pichani ni maandishi ambayo authorities zilipitisha tuyaweke kwenye jiwe la msingi. Kwa kuwa Mzee wangu Magufuli alishapitisha hili, tunakusudia kwamba jiwe la msingi katika ofisi yetu libaki kwamba yeye ndio alizindua jengo letu. Nitafanya hivyo iwapo mamlaka husika zitaona kwamba sikiuki itifaki yoyote.

Mwisho : Nina hakika Rais @sami_suluhu_hassan atatupeleka katika Tanzania aliyotamani hayati Magufuli. Sisi #EFMnaTVE tutashirikiana naye kwa ari na nguvu kubwa.


#RipMagufuli #RIPMzeeWangu #AsanteKwaYote”
 
Back
Top Bottom