Major general Suheil el Hassan, jasiri, mbabe, wanavita, mwanasaikolojia, na Rambo halisi wa kivita vitani Syria

Major general Suheil el Hassan, jasiri, mbabe, wanavita, mwanasaikolojia, na Rambo halisi wa kivita vitani Syria

Sela Son

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,120
Reaction score
7,317
SEHEMU YA KWANZA.

Kwa wapenda filamu wengi Africa na duniani kote jina la Rambo ni jina maarufu mkombozi wa wanyonge dhidi ya tawala za kibabe za Vietcong ndani ya Vietnam na hata kule Cambodia.

John Rambo ni Askari asie mzaha na mswalie mtume dhidi ya adui zake. Huwasambaratisha adui zake kwa silaha nzito na ndogondogo na Mara nyingine akiteka silaha kutoka kwa maadui zake na kuzitumia hizohizo kuwashambulia na kuwamaliza kikatili.

Haya sasa nimeanza kukumbuka hili la John Rambo nikitumia kama mfano tu wa hadithi ya kweli ninayotaka kukuhadithia kuhusu Rambo halisi wa Ki- Syria kwa jina Meja jenerali Suheil Al Hassan.
Tuendelee.

*******
Wakati wa anguko kuu la serikali ya Syria likiwa wazi katika mwaka 2011 Ni wakati huu ambapo nchi zingine za kiarabu hasa Anti US zilikuwa Tayari zimeangushwa na maandamano makubwa ya kimapinduzi kuanzia kule Libya, Tunisia, Misri, na Yemen.

Syria ya miaka ile ilishachafuka kwa maandamano ya kutisha. Waandamanaji wakidai rushwa imetawala, umaskini umetamalaki na pia swala la kukosekana kwa demokrasia na vifungo juu ya vyombo vya habari na wanahabari . Kwa sababu hizo chache kati ya nyingi miongoni mwa waandamanaji wakaanzisha uasi.

Wakaanza kuiba, kuvunja magereza na kuwatoa wafungwa. Isitoshe wananchi hawa wenye hasira kali wakaanza kuua polisi na wanajeshi watiifu wa rais Dr Bashar Al Assad wakishinikiza Rais Assad atoke madarakani kwa kujiuzulu.

Na kwa kuhofia anguko kama la Ghadafi na Mubarak Dr Assad akaanzisha mashambulizi dhidi ya raia akiwaua kwa silaha za kivita Kama ndegevita na magari yasiyopitisha risasi. Hapo wakauawa makumi na pengine mamia ya waandamanaji. Jambo Hili lilikua ni kosa kuu! Assad alikuwa ameshindwa kujifunza kutokana na makosa ya wenzake akina Ghadafi.

Walichokitaka wamagharibi kilikua kinaelekea kutimia. Mwali wao yaani Assad aliingia tayari kwenye kilengeo cha NATO. Bila kujua alishajichanganya. Lakini pengine si kujichanganya tu kimahesabu lakini ulikuwa tayari ni mkakati wa NATO wa namna ya kumuondoa Rais Assad madarakani. Matumizi makubwa ya nguvu dhidi ya raia yakawa ni kisingizio kipya cha NATO kujiingiza katika Syria kwa namna ya ufadhili wa silaha na fedha kwa vikundi vya kijihadi ili kupambana na Assad.

Humo ndimo yalimoanza kuzaliwa makundi ya kigaidi na kiasi kama FSA ( Free Syrian Army) Alqaida ( Alnusra) na baadae IS na vingine vingi.

Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2011 Syria yote ilikuwa imekamatwa na waasi na magaidi kasoro vitongoji kadhaa tu jijini Damascus.

Syria Sasa ilikuwa imengia katika full scale war. Vita dhidi ya Waasi na magaidi wanaofadhiliwa na Wamagharibi. Makambi ya kijeshi yalikuwa tayari yameangukia chini ya vikundi vya waasi. Kwa Vita ya ghafla Kama hii dhidi ya wananchi wenye silaha nzito na fedha jeshi la Syria likafeli vibaya kuzuia upinzani huu licha ya kuwa pengine na silaha bora kuliko Waasi. Jeshi liliingia katika mparaganyiko mkubwa yaani hapakuwa na connection nzuri ya utoaji wa amri kijeshi katika kamandi zote za jeshi la Syria yaani ardhini, makini na angani. Walikuwa hawajajiandaa dhidi ya uasi mkubwa hivi.

Syria ikachafuka zaidi mapambano yakapamba Moto huko Allepo,Afrin na kwingineko. Kama ujuavyo waasi na magaidi wapiganapo huja mstari wa mbele kwa morali kali. Hata wakidondoka wenzao mamia kikubwa hua ni kutimiza lengo .

Hapa Askari wenye mioyo laini nao wakaasi wakaamua kulipwa na Marekani. Nani afe kizembe? Wakati ili usiuawe ni vyema kujiunga na waasi?

Sasa basi kwa hofu na spidi kubwa makamanda wa jeshi la Assad wakaasi wakaanza kupigana dhidi ya Assad na serikali yake. Mfano wa kambi za jimbo la mpakani na Uturuki yaani Afrin ziliasi na kuwa kambi kuu za uasi na pia zikipata msaada wa hali na mali kutoka Uturuki. Wakapata anti- tank rocket, wakapata vyakula na hata inteligensia.

Pigo lililoje kwa Assad na serikali yake? Makamanda walioapa kuilinda Syria na Rais Assad wamemsaliti? Askari watiifu wakauawa kikatili kwa mamia ya makundi kwa risasi za waasi. Katika siku fulani mwishoni mwa mwaka 2011 askarijeshi watiifu kwa Assad wapatao 250 walipigwa risasi hadharani mjini Allepo na waasi waungwao mkono na Uturuki. Happ Allepo ndipo palipokua ngome kuu ya waasi na uasi dhidi ya Assad. Hilo la mauaji lilifanywa kwa makusudi kama kitisho kumuonesha Assad na jeshi lake kwamba wakijitia uhayawani kupigana watakwisha.

Kwa hali ile nani angebaki mtiifu kwa serikali iliyoitwa ya kidikteta? Hakuna! Hata hivyo Askari wengine walishaiva vilivyo. Syria ilikuwa na itakuwa kwao daima. Wakaamua kupigana kiume na kufia huko! Miongoni mwao askari hawa kulikua na mwamba mmoja mfupi si mfupi mrefu si mrefu wa saizi ya kati. Alipenda kujiita na hupenda kuitwa " "Al Nimri" ama kwa kipare "Tiger". Huyo jina lake kabisa aliitwa Colonel Suheil Salman Al Hassan. Ni nani huyu Suheil Al Hassan kivita. Ukurasa ujao tutamchimba kiundani zaidi.

ITAENDELEA...
 
SEHEMU YA PILI.

Hello Wanajf nina furaha tele kuendelea tena kuwahadithia hadithi ya kweli ya bwanavita Meja jenerali Suheil Al Hassan.

Huyu Suhel Al Hassan alizaliwa mnamo mwaka 1970 katika jiji la Latakia huko nchini Syria. Inasemwa utotoni alipenda sana ujeshi hivyo katika miaka ya ya ujana wake aliingia jeshini katika chuo cha kijeshi cha maofisa mjini Damascus.Humo alijifunza mengi ya kijeshi ikiwemo Mambo ya majeshi ya anga, na masomo ya Anti-aircraft missiles ambapo alihitimu yapata mwaka 1991 akiwa kama first class Leutenant yaani nyota moja. Baada ya hapo akafanya kazi kama mkufunzi wa elimu yake kwa miaka kadhaa akizunguka huku na huko nchini humo.

Katika miaka hiyohiyo ya 1990 alijiunga na mafunzo maalum ya special operation forces yaani ukomando. Humo akafanikiwa kuwa mwanafunzi bora miongoni mwa waliohudhuria mafunzo yale. Leutenant Al Hassan chuoni humo alikuwa kijana mpole, mwenye nidhamu ya hali ya juu, mpenda mazoezi ya viungo lakini pia mwelewa sana wa maswala ya kivita. Inasemwa pia Suheil Al Hassan alikuwa akipenda kusoma vitabu vya wanasiasa na mashujaa wa kipindi kilichopita akina General Erwin Rommel, General Zhukov, akina Gamal Nasser na wengine.

Alipohitimu yaani kati ya mwaka 1992 na 1993 akafanywa kuwa mkufunzi wa special operation forces ( ukomando) kote nchini Syria akiwapika vijana kuwa walinzi wa taifa lao.

*********
Tuendelee. Katika kipindi ambapo makamanda wakuu wengi wa Syria wakiwa wameshindwa kuunganisha ( organization) kamandi ya vikosi vya Syria yaani anga, ardhini, na majini hivyo nchi kuangukia mikononi mwa waasi na magaidi, ndipo kipindi hiki nyota ya kijana mmoja mwanavita ilikuwa ikiibuka kwa kasi ya kimbunga.

Kwa kipindi hiki aliitwa Colonel Suheil Salman Al Hassan. Mnamo mwaka 2011 kwa msaada wa Iran division ya special operation forces ilianzishwa. Division ama kikundi hiki kikaitwa 25th special mission division forces kikiwa na idadi ya Askari 900 kwa mujibu wa vyanzo vya kimagharibi. Kikosi hiki kilianzishwa lengo ikiwa Ni uamuzi wa kupigana kufa kupona . Kwani Kama vita tayari ipo kwao na lazima loyalist wa Assad wapigane kuirudisha ardhi ya Syria mikononi mwa Serikali ya Damascus. Sasa basi kikosi hiki akakabidhiwa colonel Suhel Al Hassan kukiongoza.

Hivyo kwa kuteuliwa huko Suheil Al Hassan akatoka katika ukufunzi wa ukomando na yeye Kama komando ikabidi aingie mstari wa mbele kupigana dhidi ya maadui wapya wa ndani ambao ni magaidi na waasi. Unaona hiyo sasa mwalimu anaingia vitani kufanya vita kwa namna ya vitendo zaidi kuliko nadharia.
Je mkufunzi huyu atafanikiwa? Ha ha tutaona.Kwa maandishi haya wengine wanajua pengine tumelikaribia neno la kukera yaani "ITAENDELEA". Hapana bado sana. Ndo kwanza tunaanza au sio?

Baada tu ya kuingia uongozini Colonel ( tamka kanali) Suheil Al Hassan hakupaparika kuanza kupigana bila mikakati. Akatumia akili kubwa kupanga mikakati thabiti ya kupigana kwa kuanza kuunganisha kamandi zote za jeshi la Syria yaani majini, angani na ardhini.Kwa mikakati hii migumu katika kipindi hiki kigumu wamagharibi wakampachika jina Syrian Erwin Rommel. Unamjua Generali Erwin Rommel asee? Sawa. Erwin Rommel alikuwa kamanda hatari wa kijerumani aliyeshinda Operation zote alizopewa kutimiza wakati wa Vita ya kwanza na ya pili ya dunia. Uzima ukiwepo nitakuja na uzi wake bwana huyu. Amyna.

Tunaendelea. Akili hapa ilitakiwa kutumika. Vita si lelemama. Bila akili nchi ilikuwa ikielekea kutwaliwa na vibaraka wa Marekani na wenzie! Hivyo basi, kwa sababu tayari alikuwa mtaalamu wa majeshi ya anga, pia mtaalamu waa majeshi ya ardhini kivita swala hapa likabaki moja kutambuana na kuunganisha kamandi zote za jeshi la Syria kuwa kitu kimoja dhidi ya adui ambae Ni Western paid Mercenaries.

Sababu nyingine ya kutaka organization hii ilikuwa kuepuka friendly fire. Kutokana na ukosefu wa organization na kutotambuana vikosi vya Syria Mara nyingine vilikuwa vikirushiana makombora na kuuana wao kwa wao. Jukumu Hili colonel Suheil Salman Al Hassan alilimaliza mwishoni mwa mwaka 2011 hivyo basi vita ukombozi ikawa jukumu na lengo kuu.Waasi wafe au wasalimu amri Kwamba wameshindwa.

Umeona Sasa? Operation haijaanza jeshi la Syria chini ya Colonel Suheil Al Hassan limejipanga vyema kuanza mashambulizi. Je litafanikiwa? Hello wanajf naelekea kucheki mechi Ya Simba huko kitaa hivyo basi naomba kusema hivi.

ITAENDELEA....
 
Back
Top Bottom