sikiliza hii
===
Wakati mamlaka nchini Kenya zikiendelea kutambua makaburi waliozikwa waumini wa Mchungaji, Paul Mackenzie, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Paulo Chacha ameibaini kuwepo kwa kanisa linaloendesha ibada tata.
Chacha amebaini kuwepo kanisa hilo juzi Juni 8, 2023 katika Kijiji cha Nyamayinza Kata ya Gulumungu wilayani humo ambapo amesema kanisa hilo linamilikiwa na William Masuma na mkewe, Kabula Lushika ambao wanawatoza wagonjwa Sh30, 000 kabla ya kuwafanyia maombi hayo.
Amesema wamebaini kuwepo wagonjwa zaidi ya 200 waliolazwa huku zaidi ya 50 walio taabani wakiendelea kupatiwa matibabu katika mazingira duni huku akiagiza Jeshi la Polisi kufanya chunguzi ili kubaini iwapo kuna wagonjwa waliofariki na kuzikwa eneo hilo kinyemela sambamba na kusitisha huduma za kanisa hilo.
Hata hivyo akizungumza chini ya ulinzi wa Polisi, Mhubiri Masuma amesema pamoia na kuwa na kibali cha kutoa huduma ya Tiba Asili, katika eneo hilo anatoa huduma ya maombezi kwa wagonjwa pekee huku akisisitiza kuwa hakuna mgoniwa ambaye amezuiwa kwenda hospitalini.
Chanzo: Mwananchi