David Kafulila ameteuliwa Kuwa Kamishna Idara ya Ubia kati ya sekta ya Umma na sekta Binafsi ambayo ni miongoni mwa Idara za Wizara ya Fedha na Mipango.
Majukumu ya Idara ya PPP:
1. Kusimamia, kuchambua na kuzishauri Mamlaka za Serikali katika uanzishwaji, uchambuzi na utekelezaji wa miradi ya PPP kulingana na Sheria ya PPP Sura 103;
2. Kuratibu maandalizi na mapitio ya Sera, Sheria, Mikataba na Miongozo ya utekelezaji wa PPP.
3. Kuchambua masuala ya kifedha kwenye miradi ya PPP inayohitaji fedha, msaada wa Serikali au masuala yoyote ya kisera;
4. Kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa vihatarishi na masuala mengine ya kifedha katika utekelezaji wa miradi ya PPP
5. Kuandaa kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Ubia kwa mujibu wa Sheria ya PPP;
6. Kuandaa Mfumo wa ufuatiliaji na tathmini katika miradi ya PPP
7. Kuratibu ufuatiliaji na tathmini ya miradi inayotekelezwa na Mamlaka za Serikali kwa utaratibu wa PPP; na
8. Kuandaa na kutekeleza programu ya kujenga uwezo wa PPP.