Pre GE2025 Majukumu ya nyumbani kikwazo kwa wanawake kuingia katika uongozi Zanzibar

Pre GE2025 Majukumu ya nyumbani kikwazo kwa wanawake kuingia katika uongozi Zanzibar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Joined
Oct 8, 2024
Posts
8
Reaction score
5
___.jpg

Na Thuwaiba Habibu, Zanzibar.

Sensa ya watu na makaazi ya
mwaka 2022 inaonesha Zanzibar ina watu 1,889,773 kati ya hao wanaume ni 915 ,492 huku wanawake ni 974 ,281 hii ikimanisha wanawake ni wengi.

Kwa wingi wote huo nafasi ya za kuongozi kwa wanawake bado hajakidhi malengo Kutokana na vikwazo mbali mbali ikiwemo majukumu ya nyumbani Fatma Ali anaelezea hili.

Alikuwa Mjumbe wa Kamati Tekelezaji Wadi ya Kisauni katika Chama Cha Mapinduzi CCM ni mwenye (umri wa miaka 31)mama wa mtoto ,(1) amesema nilikuwa kiongozi mnamo mwaka 2018 kabla sijaingia katika ndoa ila baada ya kufunga ndoa mwaka 2021 niachana na uongozi kwa sababu ya majukumu ya nyumbani kwani pirika zangu na za kwenye Uongozi zilikuwa zinaingiliana.

"Mwanzoni kabla ya kuolewa nilidhani naweza kumudu majukumu yote ya uongozi na ya kwenye familia lakini baada ya kuingia nikawa nimeegemea kumoja ambapo ni nyumbani ili kutimiza msingi ya ndoa"
Unapokuwa ndio kwanza kiongozi mchanga ndio unajitafuta sasa inakuwa shida kumudu majukumu yote kwasababu unataka kuwa kiongozi lakini huna uwezo wa pesa za kutafuta mfanya kazi wa kukusaidia lakini kwa walikuwa wameshafanikiwa wanamudu hilo na wengine wana watoto wakubwa kwao inakuwa rahisi.

Kupata taarifa na matukio kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Ilifika wakati nilikuwa mtoro sana katika vikao na viongozi wenzangu ilipekea nionekane nina dharau nilikuwa nalazimisha muda ambao sina kazi yaani jioni ndio kufanyike kwa pirika za kiuongozi lakini baadhi ya majukumu lazima yatekelezwe kwa wakati maalamu na sio ninaotaka."

Hii yote inasababishwa na kukosa waume waelewa kwenye masuala haya kwani wapo wanaume ambao tayari wamejitoa kwa wanawake kushiriki katika uongozi kwa kukielewa kile ambacho wanakifanya na kuwasaidia katika baadhi ya majukumu na kujuwa nini wanapitia katika uongozi lakini baadhi yao hawaelewi majukumu yaliyopo katika shughuli za kiuongozi ni makubwa na mwanamke anahitaji mapumziko hii inapelekea kuacha kumoja ambapo ni kwenye uongozi,

"Mwanawake tunakosa uwadilifu katika kitu kimoja hasa Uongozi na tunaamua kuwachilia ili kutimiza majukumu ya nyumbani kwani huona ndoa ni muhimu zaidi" alieleza fatma

Ningeomba viongozi wanawake wazoefu watupe mbinu zao wanazozitumia ili tuweze kufanikiwa kwa pamoja katika hili kwani kuna wenzetu ambao wameshindwa kama sisi katika hili.
"Tupatiwe njia za kupitia na mbinu za kufanya kwani kuna wengi naamini wameshindwa kutokana na majukumu kuwa mengi kiupande wao japo historia vipi waliweza ili tuige mifano yao"

Mariam Mbaruk khamis (umri miaka 44) Mkaazi wa kijiji Cha Mwera Kwa kozi mama wa watoto wanne amesema alikuwa na ndoto ya kuwa kiongozi ambayo ndoto hiyo ikikwama alipoingia katika ndoa kwani aliopewa rushusa feki ambayo ilikuwa inampa matumaini lakini hakuweza kufikia katika ndoto zake .

Aliolewa akiwa na miaka 20 ambapo mume wake alimpa nafasi ya kushiriki katika uongozi ila kwa sharti la kumaliza pirika za nyumbani ambapo alijuwa fika katika nyumba yake kuna kazi ambazo zitamkosesha mda wa kushiriki masuala hayo.

Soma Pia kwa taarifa zaidi zinazowahusu wanawake kipindi hichi cha uchaguzi: Kipindi hiki cha Uchaguzi wanawake wanapata nafasi ya kutosha kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi?

"Wanaume hutuziya kuwa viongozi bila ya kujijuwa kwa kutuwekea vikwazo cha kumaliza kazi za nyumbani ndio ufanye uongozi "alieleza mariam

Anafafanua kuwa majukumu ya nyumba hasa yakiwa ni mengi yanafanya akili kuchoka sana na hata ukishiriki katika uongozi nako kukiwa na majukumu unashindwa kumudu kutokana na kushoka kimwili na kiakili.

"Wewe wenywe bila kukatazwa unaamua kupumzika na kupoteza ndoto ulizo nazo za kuwa kiongozi na husababishwa na waume "
Wao hutaka kuonekana wema na hukimbia lawama kutoka kwa walimwengu kwa kuwazidi akili wanawake kwa kuwapa ruhusa na kukisirisha majukumu wanayohisi hawatamaliza na kushiriki uongozi.

" Hujiamini hasa kutokana na shughuli zilipo nyumbani kwake basi mwanamke atabaki hata jishughulisha na siasa"
Kwa mujibu wa itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC) ambayo mkataba wake ulitiwa saini mwaka 2008 inaeleza kutaka kuondoa utafauti na kuwatenga wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kusaidia kuwepo usawa wa kijinsia katika nchi wanachama na kufikia asilimia 50/50 kwenye maamuzi, serikali na taasisi binafsi

Katibu wa UVCCM Tawi la Tomondo Abdallah hamad amesema vijana wa kike wengi wanajitoa katika uongozi wanapoolewa na wengi sababu zao ni kuwepo kwa majukumu mengi majumbani mwao na ndio tunawakosa wale vijana wenye uwezo wa kuwa vipngozi bora.
"Tunapoteza vijana wa kike viongozi kutokana na majukumu hasa wanapoolewa huwa hawahudhurii tena kwenye majukumu ya vyama."

Kuwe na elimu ya kuwapa hamasa vijana wakiume tuliokuwa nao katika maeneo yetu kuwa pamoja na wake zao kwani wao ndio wa kwanza kuwaekea vipingamizi vya kumaliza majukumu ya nyumban ndipo kujishulisha na Uongozi na wengine hukataa kabisa.

"Bado vijana ndio wanataka kuonekana ni waumme wa kweli kweli kwa kuwazuiya wanawake kuweza kuwa viongozi "

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA-ZNZ, Dkt Mzuri Issa, amesema umefika wakati kuondoa vikwazo vyote vinavyo kwamisha usawa wenye hadhi sawa kwa wanawake ili kuongeza idadi ya Wawakilishi wanawake katika uongozi
amesema muda mrefu wanawake wamekua na nafasi ndogo katika uongozi ngazi za maamuzi na ndio maana waliamua kuwajengea uwezo na kuwashajiisha watumie fursa ziliopo kugombea uongozi.

Amesema TAMWA iliamua kufanya baada ya kuona Tanzania ina vijana wa kike wenye uwezo wa kuongoza , lakini wanakabiliwa na vikwazo vingi katika safari ya kufikia huko na hili limeonekana wazi katika uchaguzi mkuu.
Katiba ya Zanzibar ya 1984, imeweka wazi kuwa kila Mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu na yanayohusu taifa lake na katika marekebisho ya 2010 imeeleza kutakuwa na wajumbe BLW kwa idadi ya asilimia 40 wa wajumbe kwa kila jinsia.

Mfanya Biashara ya Kuuza Duka kutoka Mwera Hawaii Mohammed Omari Rashid amesema wanawake wenyewe hushindwa kujipangia majukumu yao,na kukosa wanaume waelewa kujuwa kuwa mkewe anatafuta na yupo na wakati mgumu ili kumsaidia ndio wanapekea kushindwa kuwa viongozi.

"Wanaume ndio vipindamizi vikubwa vya kwani huwa na maneno ya kuwarejesha nyuma wanawake kutokana na wivu na kutumia urijali wao kuwapa masharti magumu wenzao"

Katibu wa Wazazi Tawi La Mfenesini Lipi Silima Juma amesema kuwa majukumu ya nyumbani sio kikwazo kwa wanawake kukosa kushiriki nafasi za uongozi kwani wengi hushindwa kutokana na kitokujipangia majukumu yao kwani upo uwezo wa wakuandaa pirika zao na wakirudi kutekeleza.

"Wanawake viongozi hutumia muda kama dhahabu kwa kukipangia muda wa kazi na majukumu ya nyumbani"

Wanaumme huwatumia wanawake ambao wanaulewa mdogo katika ya uongozi kuwakwamisha tu lakini inawezekana wanamke kutimiza majukumu yote kwa wakati uliosahihi hio hiyo hufanywa kwa kuwanyima fursa tu.

"Naamini mwanamke anawezea kuwa kiongozi kwani kwa sasa tuna wanawake wanafanya kazi na wanamudu majukumu ya nyumba"

Wanamke akiona amewekewa kikwazo cha kumaliza majukumu ya nyumbani na atafute mwenziwe ambaye yuko kama wewe na anamudu shughuli za Uongozi vipi anafanya ili upate uzowefu na kuongeza idadi ya wanawake katika uongozi
"Wanamke kikwazo kisikuzuiye tafuta njia mbadala kushinda changamoto ili kufika asilimia 50 katika uongozi ifikapo 2025".

Mchambuzi wa Masuala ya mbali mbali ikiwemo ya wanawake na Uongozi Almasi Muhammed amesema kuwepo kwa majukumu nyumbani ambayo yamemuelemea mwanamke pekee yake ni kikwazo kwa wanawake kwenye Uongozi kwani wanaume wengi hutumia njia hiyo ili kuficha kama ni nafasi wanayotumia kuwakataza wanawake kuingia katika uongozi.

"Baadhi ya wanaume huwakwamisha wanawake kupitia majukumu ya nyumbani kwa kuwapa nafasi isiyo rasmi ya kushiki katika uongozi"
 
Back
Top Bottom