Majukumu yameanza kumbana kocha Ndayiragije

Majukumu yameanza kumbana kocha Ndayiragije

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kwa siku za karibuni Kocha Ndayiragije amekuwa kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars huku pia akiwa kocha mkuu wa Azam Fc.

Kwasasa kila wikiendi kocha Ndayiragije amekuwa na mechi ya kimataifa, aidha iwe kwenye klabu yake ya Azam Fc ama timu ya Taifa ya Tanzania.

Mfano, Taifa Stars alicheza na Burundi, wiki iliyofuata Azam Fc akacheza mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Wikiendi hii Stars wanacheza na Burundi, Wikiendi ijayo Azam Fc yuko kibaruani Shirikisho Afrika, na wiki inayofuata tena Stars anaenda Sudan kwenye mechi ya marudiano.

Mechi zote hizo zinamuhusu kocha Ndayiragije, hii imemfanya Kocha huyu kuzidiwa na majukumu ashindwe kujua lipi la kufanya. Ni wakati sahihi sasa, wa kushika kibarua kimoja tu. Maana wahenga waliwahi kusema mshika mawili moja humponyoka.

Mimi naona angebaki na Azam Fc yake tu.
 
Hata rafiki yangu Zuberi Katwila majukumu ya kuifundisha Ngorongoro heroes yanasababisha matokeo mabaya kwa klabu yake ya Mtibwa sugar! Tff watafute makocha wa timu zake za taifa!
 
Hata rafiki yangu Zuberi Katwila majukumu ya kuifundisha Ngorongoro heroes yanasababisha matokeo mabaya kwa klabu yake ya Mtibwa sugar! Tff watafute makocha wa timu zake za taifa!
Hakika mkuu
 
Hivi huyu jamaa hatima yake itakuaje iwapo timu yake ya Azam ikatolewa na hiyo Triangle, halafu na Taifa Stars ikatolewa na Sudan kwenye mechi zao za marudiano! Maana chini ya usimamizi wake, timu zote zimepigwa (0 - 1) nyumbani.

Bora abakie tu na timu moja kati ya hizo mbili. By the way, hivi TFF haina fedha ya kuajiri benchi la ufundi la timu za Taifa mpaka kufikia kuazima kwenye vilabu?
 
Kocha wa timu awe angalau kawahi kushinda taji la Primier League. Bongo tulitumia kigezo kipi kumpa timu ya Taifa?
 
TFF walitudanganya kama kocha wa muda, kocha huyu hana viwango kwani Taifa Star 's sio Mbao Fc ni timu gani ya taifa amefundisha?
Vya bure ni ghali wandugu! !
 
TFF walitudanganya kama kocha wa muda, kocha huyu hana viwango kwani Taifa Star 's sio Mbao Fc ni timu gani ya taifa amefundisha?
Vya bure ni ghali wandugu! !
Leo amepewa Taifa Stars rasmi. Hakika TFF imetumia vizuri ile kauli ya wahenga "Penye udhia penyeza rupia"
 
Back
Top Bottom