MAJUKWAA YA VIJANA
Kumekuwa na wimbi kubwa la mikutano, makongamano na mabaraza ambayo huandaliwa kwa ajili ya kutatua changamoto za vijana hususani katika sekta ya ajira na kujiajiri. Mabaraza hayo ambayo huandaliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na watu mashuhuri na wenye ushawishi kwa jamii, asasi za kiraia na binafsi yamekua hayana tija au hayayoi matokeo chanya katika kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili vijana katika masuala ya ajira na kujiajiri na hii ni kutokana na sababu zifuatazo:-
Mada ziandaliwazo haziwagusi walengwa, leo hii kiongozi anasimama kwenye jukwaa au mkutano wa vijana badala kuzungumzia utatuzi wa changamoto za ajira na kujiajiri, anaanza kueleza utekelezaji wa miradi ya maji, umeme, sekta ya afya n.k. Yampasa kiongozi kusimama na kueleza mipango mikakati kwa ajili ya ajira na kujiajiri kwa vijana lakini anaanza kueleza miradi mingine ya kiserikali. Hivyo kupelekea kupoteza tu muda katika mikutano hiyo ambayo huandaliwa kwa ajili ya vijana. Isitoshe kiongozi katika majukwaa haya anatumia muda mwingi kuzipamba mamlaka za juu kuliko kueleza ni mbinu gani zinaandaliwa ili kuondoa changamoto za vijana.
Watoa mada waalikwa sio uhalisia wa vijana wa mtaani, leo hii tunawachukua watu waliofanikiwa, maarufu au kutoka katika taasisi Fulani ndio wasimame kuwasemea vijana changamoto zao badala ya kusikia kutoka kwa vijana wenyewe wa hali ya chini kimaisha au wale ambao wako mtaani. Hivyo hupelekea mamlaka za serikali kutotilia mkazo matakwa ya vijana kwani huwata vijana kuiga mifano kutoka kwa wawakilishi hao (watu mashuhuri au waliofanikiwa) bila kuangalia ni changamoto gani wanapitia hawa vijana walioko mtaani.
Taasisi za vijana nyingi zimetawaliwa na uchama, katika mikutano na makongamano haya mengi hayana tija kwa sababu hii ya uchama na itikadi za kisiasa hivyo inakua ngumu kwa viongozi wa taasisi hizo au vijana wenyewe kuzungumza mambo ya msingi ambayo yatawabana viongozi wa kiserikali kwa kuhofia maslahi yao katika vyama vyao vya kisiasa. Hiyo ni mojawapo pia ya changamoto ambayo inafanya mabaraza na mikutano hiyo isiwe na tija katika kutatua changamoto za ajira na kujiajiri kwa vijana wa kitanzania.
Yanayozungumzwa kwenye mikutano na majukwaa ya vijana hayatekelezwi, kwani imekua ni kasumba ya viongozi wengi wa ngazi za juu serikalini kupanga sera za ajira kwa vijana kwenye majukwaa na mikutano hiyo bila kuifanyia kazi na kuwaacha vijana katika sintofahamu kubwa, hivyo hakuna maana ya majukwaa hayo kufanyia kwani kila kinacho zungumzwa hapo hakitekerezeki, kinaishia hapo hapo na zibaki kuwa ahadi kwa viongozi wa kiserikali na wanasiasa. Hivyo mikutano hiyo inakua inatumika kama sehemu ya kujitangaza kwa viongozi na wanasiasa na so kwa ajili ya kuwasaidia vijana wa kitanzania.
Mapendekezo
Mikutano, majukwaa na makongamano yanayoandaliwa kwa ajili ya vijana yawe na tija au chachu ya kutatua changamoto zinazo wakabili vijana hapa nchini, pawe ni mahala ambapo vijana wa kitanzania wataeleza changamoto zao na kuuliza maswali ambayo majibu yake yatatolewa kwenye mikutano au makongamano hayo. Kwani hapo ndipo huwa sehemu ya vijana kueleza matatizo yao na yakasikika kwa viongozi na serikali ujumla. Mikutano na majukwaa hayo yaweze kufungua fursa na pia yatoe mwangaza kwa vijana wa kitanzania katika kutatua changamoto zinazo wakabili ili waweze kujikwamua kwenye shimo la ajira na kujiajiri.
Hivyo basi kuna haja ya vijana wenyewe kusimama kidete na kuzipiga kelele kwa mamlaka husika za serikali kwani kufanya hivyo itaongeza hali utendaji kazi ya viongozi wa serikali katika majukumu yao hususani katika kutatua changamoto zinazohusu sekta ya vijana. Kama kijana ndio taifa la kesho iweje atelekezwe, ustawi wa kijana wa kesho upo wapi?
Vijana kuepuka kuwa na mlengo wa uchama au vyama vya kisiasa katika kufanikisha malengo yao, kwani kufanya hivyo itapelekea vijana kuwa na kauli moja katika kutatua changamoto zinazo wakabili hasa hasa katika sekta ya kujiajiri. Kugawanyika kwa vijana kupitia itikadi zao za kisiasa ndio chanzo cha matatizo yao kutofanyiwa kazi kwa weredi zaidi na mamlaka husika hapa nchini.
Vijana ni rasilimali ambayo imekuwa ikitelekezwa na ikitumika Kama ngazi kwa wanasiasa na viongozi wa serikali katika kuyafikia malengo yao lakini kama rasilimali hii ingetengezewa mikakati mizuri Tanzania na dunia kwa ujumla ingeshudia maendeleo makubwa sana kwa vijana hawa wa kitanzania lakini wamekuwa wa kuhangaika na maswali yao yakikosa majibu sahihi .
Taifa lisipostahimili ustawi wa vijana, Basi taifa hilo huanguka. Vijana wako majumbani tu na mitaani bila ya matarajio yoyote yale ya maisha yao, wanasiasa na viongozi wa serikali wasafishe njia na dhamira zao kwa vijana ili kuondoa mitazamo hasi katika maisha ya kawaida ya vijana wa sasa. Kwani kufanya hivyo kutaonesha uwajibikaji na utawala bora kwa serikali iliyopo madarakani.

Upvote
0