ABTHEGREAT
New Member
- Jul 27, 2022
- 4
- 6
Kuna msemo mmoja wa kiswahili unaosema"MAJUTO NI MJUKUU"bila shaka wote tumeshawahi kuusikia.
Majuto ni maumivu yanayozalishwa kwa kutotumia wakati na nafasi kwa usahihi na Mjukuu ni matokeo yanayotokana na kutotumia wakati na nafasi kwa usahihi.
Kama ilivyo kwenye maeneo mengine ya kimaisha chuoni pia Majuto huzalishwa.
Majuto yamebebwa na Ninge......na yamezaliwa na Nita.
"Nitasoma kesho.....Ningejua ningesoma Jana"
Wahitimu wengi wa vyuo wanayomajuto mengi ambayo nimeona ni vema nikakushirikisha ili usifanye makosa kama waliyoyafanya wahitimu wengi.
(Majuto haya ni zao la tafiti niliyoifanya kwa kuzungumza na wahitimu zaidi ya 100,Kote nchini Tanzania mwaka 2019)
N:B Majina niliyoyatumia kwenye andiko hili si majina halisi ya watu niliohojiana nao)
1.Ningejua ningesoma kwa bidii ili nipate matokeo mazuri.
Aina hii ya majuto ilitolewa karibu na asilimia 60% ya watu niliowafanyia mahojiano.
Watu hawa wanasema hawakutilia maanani Sana swala la kujibidisha kimasomo kwa sababu mbalimbali. Moja ya sababu zilizotajwa na wengi ni Kuwekeza muda mwingi kwenye mahusiano yasiyo na tija na kwa kufanya starehe zilizopindukia.
Dada mmoja alisema Nilitumia muda mwingi kuyamwagilia maji mahusiano yangu na Chris, Nilijitoa kwa ajili yake kuna siku sikwenda hata darasani lakini Mwisho wa siku Chris alinisaliti. Nilidhoofika sana kwa Kumuwaza, Hii iliniathiri Maana nilikosa vyote Mahusiano na matokeo mazuri ambayo yangenisaidia kujiendeleza zaidi.
Kenny naye anasema ninatamani kujiongezea elimu ila siwezi kwa sababu G.P.A yangu ni ndogo siwezi kuendelea mbele”
Ni ukweli usiopingika kuwa tunapofika vyuoni tayari tushakuwa watu wazima na tunauhuru wa kufanya kila tunalolitaka Ila tusisahau kuwa sisi ni watu muhimu kwa Taifa na familia zetu,
Hivyo tujitahidi kufanya kila jambo kwa kusudi na wakati sahihi
Ni lazima tuijue thamani yetu na sababu ya sisi kuwepo tulipo Sasa,Tunakumbushwa kwenye kitabu cha Mhubiri 3:1-3
Wekeza muda mwingi kwenye lengo mama lililokuleta Kwanza hapo chuoni' ambalo ni masomo kisha mengine yatafuata
2.Ningejua ningeweka Akiba.
Kaka Elly aliniambia “Ningejua kwenye bumu langu ningekuwa hata naweka akiba ya Tsh.elfu hamsini kwa kila bumu zingenisaidia, Ningeanzisha hata kibiashara kidogo Ila sikuweka chochote.
Wanafunzi wengi wa chuo wanasifika sana kwa umiliki wa vitu vya thamani Kama vile simu, Nguo n.k.na kwa kufanya starehe zilizopindukia.Vitu visivyodumu kwao, Vitu vinavyowapa heshima ya muonekano lakini aibu ya mifukoni.
Siwazuii Kumiliki vitu vya thamani wala kufanya starehe lakini nawakumbusha pia kuweka Akiba kwa ajili ya kesho.Kuna maisha baada ya chuo,Suala la Ajira ni changamoto, Hivyo badala ya kuanza kuombaomba mtaji kwa watu au kutafuta kazi, Akiba yako inaweza ikawa ni chanzo kikubwa cha mtaji.
Jibane, Jiwekee kidogokidogo, Usiweke vyote kwenye Matumizi, Jifunze kuwa na Nidhamu ya fedha. Kuwa na Bajeti, Bajeti yako itakusaidia kuishi vyema na kuweka akiba.
3.Ningejua ningetengeneza Mtandao wa watu wenye tija.
Dada Hadija Dida Biriani Aliniambia “Moja kati ya vitu ninavyovijutia nilipokuwa chuoni, Sikutengeneza Mtandao utakaonisaidia baada ya kuhitimu unaohusiana na Taaluma yangu"
Watu wengi wanapokuwa vyuoni hugeuka visiwa hujiona kuwa wanakila kitu, Hivyo hawawahitaji wengine.
Jitahidi sana unapokuwa chuo, Utengeneze mtandao wenye tija.
Wanafunzi mnaosoma nao kozi moja, Mnaoshea vipaji n.k Tengeneza nao mahusiano mazuri. Mahusiano hayo yatakuja kukusaidia baadaye.
4.Natamani ningeishi Maisha yangu.
Adolph anasema "Bro niliigaiga sana, Sikuishi uhalisia wangu nilijifananisha na kutaka kushindana na wengine wanaonizidi kipato, Mwisho wake nimetoka chuo bila chochote"
Groly pia anasema Dah! pengine Nisingeathirika na Ugonjwa wa UKIMWI kama ningerizika na maisha yangu. Tamaa yangu yakumiliki nguo za gharama, Marashi Na simu Ili nilingane Na rafiki zangu imeniponza, Ilinibidi kuuza mwili wangu ili nivipate vyote hivi.”waambie wadada wenzangu waishi maisha yao
Humphrey Kijana aliyesoma uhandisi na kupata Matokeo makubwa lakini Sasa Ni Mrahibu wa madawa ya kulevya a.k.a Teja aliniambia"Kampani,Kampani mbaya Sana Mwanangu,niliwafuata Sana marafiki mwisho nimeishia kuwa Teja,Siwezi kuishi bila madawa,pombe wala bangi,Kuna wakati akili huwa zinanirudia natamani niwe Kama zamani nitimize ndoto zangu,Ila ndo basi siwezi tena"
5.Ningejua ningekifanyia kazi kipaji changu
"Kaka mimi ni mchoraji mzuri sana Ila sikukifanyia kazi kipaji changu nikiwa chuo naumia sana kuona leo hii Kuna watu niliokuwa nawazidi uwezo wamefika mbali" aliniambia maneno haya rafiki yangu Matata.
"Mimi ni muimbaji nimemalizia chuo mwaka juzi ila napata ugumu sana kupata opportunities za kunifikisha mbali kila nikijaribu nakutana na vikwazo,Najuta laiti ningejua ningepambana zaidi nikiwa chuoni' maaana Ni rahisi kupata opportunities kule" hayo aliniambia rafiki yangu Quuen Rozy
"Nilikuwa na uhakika na ajira kwa kuwa nilikuwa nasomea kozi ya udaktari Ila baada ya kumaliza nimegundua Mambo sivyo yalivyo nawashauri waliopo bado vyuoni wasome kwa bidii,Wajifunze vitu vingine nje ya Elimu ya Darasani na wavitumie vipaji vyao"aliniambia Rafiki yangu Daktari Hussein.
6.Ningejua nigehudhuria Semina na Makongamano yale kuna watu yamewasaidia.
Asha Anasema “Niliposikia yapo makongamano na semina mbalimbali sikutilia maanani, Kiukweli nilijisemea kabisa Hakuna lolote jipya huko, Hawana la kuniambia, Kumbe nilijidanganya Leo kuna rafiki zangu wamefaidika na semina zile bwana"
Kujifunza ni hitaji la msingi sana kwa mtu yoyote yule ambaye anataka Mafanikio.
Suala la kujifunza ni endelevu, Anayedhani anajua kila kitu huyo ni mjinga.
7.Ningejua nisingesoma kozi hii
"Ni kweli nimekuwa daktari ila sio aina ya kazi ninayoipenda,nilisoma kwa kuwa baba aliniambia niisome"
"Kaka ninaifanya kazi hii lakini sina furaha kabisa,ilinibidi niisome kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa kupata mkopo"
Hayo ni baadhi ya maneno niliyoambiwa na wahitimu mbali mbali.
watu wengi wapo sehemu zisizo sahihi kwa sababu walisoma kozi zisizo sahihi.
wanafanya kazi kwa majuto na maumivu makubwa,Wewe uliyepo chuoni chukua hatua leo,ushinde mtego wa kuwa mtumwa maisha yako yote.
HITIMISHO
Dah! Ama kweli majuto ni majukumu, Wewe uliyepata nafasi ya kuyajua majuto haya ungali chuoni bado ni nafasi njema uliyoipata ya kuyajua makosa waliyoyafanya wengine na wakajuta,
Hata kama kuna makosa pia unayoyafanya/uliyoyafanya mwenyewe huu ni wakati wa kujisahihisha, kujisamehe na kusonga mbele.
Chukua hatua kuyaepuka Kwa kufanya yakupasayo kwa wakati huo ukiwa chuoni.
Kumbuka usipoziba ufa leo, Kesho utajenga ukuta

Upvote
7