Uliza_Bei
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 3,216
- 990
Jamani naomba kuwaletea ukweli huu: makaa ya mawe ndiyo nishati inayoongoza duniani kwa kutoa umeme hasa katika nchi zilizoendelea ikifuatiwa na hizi zingine za nyuklia, maji na hata non renewables kama umemejua. Tanzania tuna reserve kubwa sana ya makaa ya mawe, waulizeni wataalam wa nchi hii watawaambia. ni aibu kubwa mpaka sasa hatujaanza kutumia nishati hii wakati waziri anajua hili kaambiwa na wataalam na hata JK namshangaa kama hajui na kama anajua kwanini ananyamaza wakati hawa vigogo wanaendelea kutengeneza pesa kifisadi katika majenerata na umeme wa maji usiokuwa na tija wala nafuu? Wananchi wenzangu tuamke tupige kelele....Stamico kama wanasema kwenye mafaili tunawaomba waseme hata kwenye jamii kama njia ya kushitakia ktk jamii ili tatizo la umeme liishe nchini.