Makabila ya Tanzania: Tamaduni zao na Historia yao

Wakurya ni wachapakazi.....wataftaji.... Sio wavivu.... Wana wivu sana na wakipenda wanakabidhi mwili na roho...hawakati tamaa....watu wa kujitolea
Wana adabu na usipokua na adabu mboko zinakuhusu

Ukiwakosea wanakufunza adabu(ngumi mkononi)
 
Abakuria (au Wakurya) ni kabila la watu wanaoishi katika wilaya za Rorya,Tarime na Serengeti kwenye mkoa wa Mara, kaskazini mwa Tanzania, na katika wilaya za magharibi na mashariki mwa Mkoa wa Nyanza katika sehemu ya kusini mashariki ya Kenya.

Mnamo mwaka 2005, idadi ya Abakuria ilikadiriwa kuwa 690,000, ikiwa ni 430,000 wanaoishi nchini Tanzania na 260,000 nchini Kenya. Lugha yao niKikuria.

Abakuria ni wakulima na wafugaji, huku Abakuria wa nchini Kenya wakiegemea sana kwa kilimo nao wa nchini Tanzania wakiegemea sana ufugaji. Hasa Abakuria walio katika wilaya ya Serengeti wanatambulika kama wafugaji.

Abakuria wanafanana na Wakisii wa nchini Kenya kwa lugha na umbile. Wanadhaniwa walikuwa kundi moja hadi waliposhambuliwa vikali naWamasai mnamo karne ya 19 na kusambaratishwa katika maeneo tofautitofauti.

Utengano huo ulisababisha kuweko kwa lahaja mbili ambazo zinaeleweka na kila kundi.

Abakuria wamegawanyika katika "makabila madogo" au koo kumi na sita, nazo ni: Nyabasi, Bakira, Bairege, Bagumbe (wanaoishi katika wilaya za nchini Kenya na Tanzania), Batimbaru, Banyamongo, Bakenye,Basimbiti, Basweta,Barenchoka, Baikoma, Bamerani na mengineyo. Makabila haya madogo yote yapo pia katika kabila la Wakisii nchini Kenya.

Kabila la Abakuria pia linakaribiana na kabila la Wazanaki katika Mkoa wa Mara nchini Tanzania. Itikadi zao kadhaa zinafanana.

Historia ya abakuria(Wakurya).
 
Mura umesema vizuri kabisa wara hujakosea neno
 
Kwa jinsi wanavyo piga wake zao, eti wakati wa kutongoza wanabeba visu, mapanga, nyundo ukiwa wakataa wanakumaliza hapo hapo
Hizo ni dhana za watu ila kumbuka mtu hawezi kukupiga bila kumkosea au bila kuwepo kwa misigano za kauli!.
(Fikri na ondoa hiyo dhana yako)
 
Kichuri ni mboga ya kikurya(mavi ya mbuzi yale ya kijan yaliyopo tumboni) hii mboga wakurya wanaipenda sana. Kama unataka kuoa sema sio kuwafahamu tu na kuwachora
Mkuu kama unawafahamu elezea kwa urefu ueleweke.
 
Mbona hakuna Mukurya yeyote ariyechangia haboo?? Akichangia mumocha tuu ntakuambieni. Hao woote wariochangia naona ni baryisia tuu na basaghani mtaiya kibharaa
 
Abakurya=abha'kurya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…