Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Leo asubuhi katika matembezi yangu Maktaba nimekuta picha ya kaburi la Sheikh Haydar Mwinyimvua (1905 - 1987) ambae mwanae Sheikh Ahmed Haydar tumemzika siku chache zilizopita.
Picha hii nilipiga mwaka wa 2017 siku ya maziko ya Kleist Abdul Sykes (1950 - 2017).
Tulikuwa tumemaliza kuzika na watu wachache tukabakia nyuma kufanya dua za ziada na nakumbuka aliyetuongoza kwenye dua ile alikuwa Sheikh Abdallah Awadh.
Tulipomaliza kusoma Adam Haydar mdogo wake Sheikh Ahmed Haydar akanivuta akanambia, ''Mohamed njoo tumsomee dua Mzee Haydar huyu hapa.''
Nyuma tu ya kaburi la Kleist ambae alikuwa kazikwa jirani na baba yake, lilikuwa kaburi la Sheikh Haydar Mwinyimvua.
Marehemu hawa wote wawili wawili walipigania uhuru wa Tanganyika na wameacha historia kubwa.