Tukiwa tunasubiri muda wa asubuhi kwenda kupiga kura katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa ambao unafanyika leo Novemba 27, 2024.
Kuna hii video imenishangaza na kujikuta nacheka na kutafakari sana. Ambapo inawaonyesha makanda wa CCM wakiwa nyumbani kwa mtu wanaosha vyombo na huku wakisema tunaomba tu kura.
Sasa inamaana wameona ndiyo njia rahisi ya kuwafikia wananchi ili wapigiwe kura za ndiyo na sio tena kupitia kwenye majukwaa na kunadi sera zao?