Zogoo da khama
JF-Expert Member
- May 20, 2013
- 631
- 592
Ndg zangu habarini za majukumu?
Naomba ushauri au msaada nini nifanye juu ya hili:
Mimi ni mjasiliamali nafanya uchuuzi na taasisi za umma na serikali, mwaka jana wote biashara haikuwa nzuri hasa baada ya mfumo mpya wa manunuzi yaani Nest kuanzishwa hivyo kupelekea ushindani kuwa mkubwa. Kimapato nilishuka sana sana. Sasq kwa upande wa makadilio kwa mwaka 2023 - 2024 nilikuwa nalipa 765,512 kila baada ya miezi mitatu hiyo nimelipa yote hadi December 2024. Sina deni, leo nimekwenda TRA kwaajili ya makadilio ya 2024-2025 naambiwa nitafute mhasibu anifanyie hesabu zangu on-line nikasema sina uwezo wa kumlipa pigeni hesabu mnipe makadilio nilipe cha ajabu makadilio yamekuwa makubwa kuliko mwaka uliopita, bahati nzuri nimeweka kumbukumbu za risiti zote nilizotoa mwaka jana woote toka January to Dec 2024. Je nini lifanye ili nilipe kadri nilivyopata? Inakuwaje pato la mwaka lishuke lakini kodi iongezeke? Ushauri ndg zangu nipate haki ya kulipa kodi kwa kile nilichovuna na sio kwa kuongezewa nisichovuna ili kufurahisha/ kukomoana.