Makadirio ya tiles kwa nyumba ya ukubwa huu mkoani Mwanza

Mlatino Zeshalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
2,237
Reaction score
3,769
Wakuu habari za majukumu,
Kama title ilivyo, naomba mnisaidie kujua makadirio yote kwa ujumla maana nimesikia ukiachana na tiles, mchanga, maji na cement, kuna kitu inaitwa grout, skating,

Ukubwa wa vyumba ni kama ifuatavyo:

Sitting Room: 525*630
Master Bedroom: 524*385
Bedroom 1: 280*410
Bedroom 2: 300*410
Kolido: 125*770
Dinning: 343*273
Toilet 1: 120*430
Toilet 2: 180*410
Store: 390*130
Kitchen: 280*273

Note: Size ya vyumba ni kwa CM.

Wakuu naombeni mnisaidie ili nijue naanzaje. Sitaweka vyote kwa wakati mmoja. Pia kama kuna fundi aliye smart anicheki ili tushauriane.

Asanteni na maandalizi mema ya sikuu za Kristmass na Mwaka mpya
 
Tafuta sqm za kila chumba. Mfano sitting room ni
5.25×6.3=33
Sitting Room yako ina sqm 33. Tuseme unaweka tiles za 40*40 ambazo box moja lina sqm 1.94
Unachukua 33÷1.94=17
Maana yake Sitting Room yako utatumia box 17 za tiles za 40*40. Tumia kanuni hii kwa kila eneo la nyumba utajua jumla ya gharama za tiles.
Cement inaenda kulingana na ukubwa wa chumba na ubora wa rough floor. Uneven surface utatumia cement nyingi. Chumba cha kawaida kinaweza kutumia mifuko mitatu. Grout sio lazima tiles zinaweza kujengwa bila gap. Kazi ya grout ni kujazwa kwenye gaps.
 
Nashukuru mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…