'Makahaba' walalamikia polisi

'Makahaba' walalamikia polisi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KenyelaPolice(1)(21).jpg

Kamanda wa polisi mkoani wa Kinondoni (RPC), Charles Kenyela.

Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, limelalamikiwa kwa vitendo vya baadhi ya askari wake kuvamia vyumba vinavyodaiwa kupangwa na watu wanaodaiwa kuwa makahaba (madanguro) na kuwapora fedha, simu na vitu vingine vya thamani nyakati za usiku.

Aidha, askari hao wamedaiwa kuwageuza wanawake hao mashine za kutolea fedha (Atm) ambapo hufika katika vyumba vyao kila baada ya wiki moja na kuwadai fedha kati ya Sh.30,000 na 50,000 kila mmoja kama hongo ili wasiwafikishe polisi.

Malalamiko hayo yametolewa na baadhi ya akina mama wanaoishi eneo la Mwananyamala walipozungumza na NIPASHE baada ya askari hao kukamata wanawake zaidi ya 87.

Kiongozi wa wanawake hao, Judith Rugamwa alidai kuwa, askari hao kutoka vituo vya Oysterbay na Mabatini wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuwapiga, jambo ambalo ni kinyume cha haki zao binadamu.

"Wakitukamata huwa wanasema kosa letu ni kufanya ukahaba, lakini tukifikishwa kortini kosa linabadilika na kuwa uzembe na uzururaji, wakati wametukamata vyumbani kwetu ," alisema Judith.

Alisema wamechoka kunyanyaswa kama wakimbizi na kuonya kuwa sasa wanajiandaa kupambana na kila askari atakayefika hasa nyakati za usiku na kuwavunjia milango ya vyumba vyao ili kuwamata na kuwalazimisha wawape fedha huku wakimtaja afande Swai na Emma kuwa ndiyo wanaoongoza uovu huo.

Akizungumzia tuhuma hizo, afande Swai alijitetea kuwa yeye binafsi hajawahi kushiriki katika kuomba fedha wala kupora simu za wanawake hao licha ya kukiri kuwa ndiye anayeongoza misako yote Kinondoni.

"Kuhusu madai ya kuomba fedha, siwezi kukataa kwa sababu mimi huwa siingii vyumbani kukamata wanawake hao, badala yake askari wangu ndiyo wanaohusika moja kwa moja kabla ya kuwaleta katika gari ambayo huwa nawasubiri, lakini kama wanafanyiwa hivyo naomba wawataje kwa majina askari hao," alisema.

Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani wa Kinondoni (RPC), Charles Kenyela, alisema amri ya kuwasaka na kuwakamata makahaba hao huwa inatolewa na ofisi yake na kwamba madai ya polisi wake kuchukua fedha na simu za watuhumiwa ni uongo mkubwa.

"Kama kuna mtu amewahi kufanyiwa hivyo aje ofisi kwangu na ushahidi ili ofisi yangu ichukue hatua kali za kinidhamu kwa sababu anayeshawishi, anayetoa na kupokea rushwa wote wanafanya makosa, waache kulalamika waje niwasilikize," alisema Kenyela.

CHANZO: NIPASHE

kitu gani kinachowafanya wanawake hao kubaki huru mitaani ilhali amri ya kuwakamata inakuwa imeshatolewa kama si kulindwa na hongo wanazoombwa! Maaskari wengi wa TZ hawana uelewa wowote juu ya kazi zao, kazi za kipolisi zipo kwaajili ya kutetea wanyonge na kukandamiza maovu na si kutumia madaraka ili kumkandamiza mwananchi.
 
Mkuu EMT na MziziMkavu:

Hivi Sheria ya Tanzania inasemaje kuhusu "ukahaba"? maana hii quote hapo chini inaonyesha kama vile ki-sheria za Tanzania ukahaba siyo "kosa":-

"Wakitukamata huwa wanasema kosa letu ni kufanya ukahaba, lakini tukifikishwa kortini kosa linabadilika na kuwa uzembe na uzururaji, wakati wametukamata vyumbani kwetu ," alisema Judith.
 
Kenyela anautaka ukamanda wa kanda maalmu kwa nguvu sana
 
Kufanya ukahaba ni kosa la jinai. Polisi wanawakamata kwa ukahaba lakini wanashindwa kuwashtaki kwa ukahaba either kwa sababu polisi ni wazembe katika kutafuta ushahidi wa ukahaba or wanafanya uchunguzi na kukosa ushahidi wa kuwashtaki na kosa la ukahaba.

Matokeo yake wanashusha kosa na kuwashtaki kwa kosa la "uzembe na uzururaji".

Lakini mie naona ni uzembe maana hata RPC wa Kinondoni kasema wazi kuwa kama kuna mtu amewahi kufanyiwa hivyo aende ofisini kwake na ushahidi ili ofisi yake ichukue hatua kali za kinidhamu.

Kama vile siku hizi kazi ya polisi imekuwa ni kukaa ofisini kama ma-executives vile wakisubiri raia wafanye uchunguzi na kuwaletea ushahidi ili polisi waweze kuchukua hatua.

Hata hivyo, inashangaza kwa mtu kushtakiwa kwa kosa la "uzembe na uzururaji" lililofanyika nyumbani mwake.
 
Mkuu EMT na MziziMkavu:

Hivi Sheria ya Tanzania inasemaje kuhusu "ukahaba"? maana hii quote hapo chini inaonyesha kama vile ki-sheria za Tanzania ukahaba siyo "kosa":-

Ndio maana wakikamatwa asubuhi inayofuata wanapelekwa mahakama ya jiji Samora, ukiangalia makosa wanayoshitakiwa nayo kama sheria unaifahamu utashangaa sana.
 
mnawakata hawa wanatafuta riziki wapeni ajira
 
polisi wangefanya hivyo kwa majambazi na mateja.wanapenda kukamata macd kwajili ni walaini!!
 
Makahaba hawa ni wale akinamama ambao wengi HUDAIWA kuwa ni wenyeji wa mkoa mmoja ulio kaskazini magharibi ya nchi yetu. kinamama hao hufanya biashara ya ngono kwa kupanga vyumba ambavyo huwa vina milango inayotazama vichochoro ambako wateja wao huitumia kuingia katika vyumba vyao. Utafiti nilioufanya mbali ya kinamama hao kuwa maeneo ya Mwananyamala wanapatikana pia maeneo ya Manzese Uwanja wa Sifa zamani uwanja wa fisi, Tandika sokoni, Temeke sudan, Temeke Sokota na maeneo ya Temeke Kata 14. Uzoefu unabainisha kuwa kinamama hao hupendwa sana na vijana wasio na wake na wenye kipato vha chini kwani hutoa huduma ya ngono kwa bei nafuu sana. Aidha, kinamama hao ni kimbilio la vijana wengi wanaobalehe. Inabainishwa kuwa kinamama hao huwa hawaruhusu fore play kabla ya game kwani kwao kufanya hivyo kwao ni kupoteza muda. Wenye nyumba wengi waliowapangisha kinamama hao wanafahamu kwa undani kuhusu biashara inayofanywa na kinamama hao lakini wamekuwa wakiifurahia kwani hupokea malipo makubwa kama wanayopata wanaowapangisha wafanyabiashara wa maduka.
 
Kenyela anautaka ukamanda wa kanda maalmu kwa nguvu sana

Ni kweli hawa maaskari wamewafanya hawa makahaba ndio ATM zao kwa kuwakamata na kuwadai hongo,inawezekana wakisha kusanya wanampelekea kiasi huyo Kenyela wao kila wiki kwani zoezi hilo hufanywa mara moja kila wiki!!
 
Kama sijakosea ni Kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Kujamiiana.

Kifungu hiki kinafanya marekebisho kifungu cha 139 cha Kanuni za Adhabu.

Mkuu hii ni section 139 (1) (a) ya Penal Code: Any person who, procures, or attempts to procure, any person, whether male or female of whatever age, whether with or without the consent that person, to become, within or outside the United Republic of Tanzania, a prostitute. Hapa sioni wanapokataza prostitution
 
Hicho kifungu ulichokitaja ni moja ya vifungu vinavyo-define prostitution.

Unless kama kuna mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni, kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Kujamiiana ambacho kilifuta kifungu 139 cha zamani cha Kanuni za Adhabu na ku-replace na kifungu kipya cha 139 kinasema kuwa prostitution hili ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 10 jela na faini isiyopungua sh 100,000 na isiyozidi sh 300,000 au vyote kwa pamoja.
 
Mkuu EMT na Ngambo Ngali nawashukuru sana,

Nadhani the bottom line ni kuruhusu - legalize - hii biashara, maana nadhani kwanza maana ya "kahaba" haitoi nafasi kwa mahakimu kumtia hatiani huyu mtu anayekamatwa na polisi kwa hatia ya "ukahaba"...! Halafu pia nadhani na upelelezi wake ni mgumu sana...!
 
Last edited by a moderator:

Hakuna haja ya kuligalize hii biashara, kwa sababu in the first place haijakatazwa, nikiangalia kifungu husika cha sharia prostitution is not an offence in Tanzania.
 
Hicho kifungu ulichokitaja ni moja ya vifungu vinavyo-define prostitution.

Unless kama kuna mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni, kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Kujamiiana ambacho kilifuta kifungu 139 cha zamani cha Kanuni za Adhabu na ku-replace na kifungu kipya cha 139 kinasema kuwa prostitution hili ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 10 jela na faini isiyopungua sh 100,000 na isiyozidi sh 300,000 au vyote kwa pamoja.

Mkuu EMT, najaribu kusoma kifungu 139 kama kilivyorekebishwa na sheria namba 4 ya mwaka 1998 bado sioni mahala wanapokataza. Nimeangalia chapter XIV yote sioni mahala wanapokataza, inanifanya nishawishike kuwa hakuna kosa la jinai la prostitution Tanzania.
 
Soma kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Kujamiiana hapa: http://www.hsph.harvard.edu/population/trafficking/tanzania.sexoffenses.98.pdf

Unataka kuniambia kuwa sheria imebadilika na kuhalalisha prostitution?
 
Back
Top Bottom