BAJETI,USTAWI WA JAMII
Na Emmanuel Ndaki
0747093133
DIRA na mwelekeo wa nchi inahusisha makadirio,mapato na matumizi,yaani tunategemea kusanya kiasi gani, tunatumia kiasi gani kujenga miundombinu ya uchumi na huduma za kijamii.
Makadirio,makusanyo na Matumizi inamuhusisha mlipa kodi,haijalishi ni taasisi, wafanyabiashara, makampuni au wawekezaji.
Kwa maelezo mafupi, bajeti inaelekeza dira ya makusanyo na Matumizi ya kile kinachokusanywa, kinachotumiwa na kinachobaki akiba kwa maslahi ya nchi.
Sio dhambi kuwa na miradi ya kimikakati,siyo dhambi hata kidogo kukopa fedha kwa aajili ya kujenga na kuboresha huduma za kijamii na miundombinu mbalimbali.
Turudi kwenye hoja kwa kudurusu vipaombele vya bajeti. Bajeti imezingati kudhibiti mfumuko wa bei,Ujenzi wa viwanda,Ajira kwa vijana,nafuu ya maisha na umasikini.
Sasa tujiulize je vipaombele hivi vimezingati ustawi wa jamii? Na BAJETI inawezaje kuudhibiti mfumuko wa bei?
Ili Bajeti iweze kudhibiti mfumuko wa bei,ni lazima iweze kuzalisha kwa tija, ,kuagiza bidhaa, kuuza na kununua.
Kupunguza Matumizi ya serikali,kuharisha malipo yasiyo yalazima,kukuza biashara huria nk.
Bajeti ikiweza kuzalisha kwa wingi itamudu mahitaji na ghalama,Bajeti ikiweza kuumpa mkulima elimu, akalima kilimo cha biashara,serikali ikanununu ama kumtafutia soko akauza,tutasema Bajeti imetekeleza kudhibiti mfumuko wa bei na imetoa unafuu wa maisha.
Kama tumeamua kuwa wajamaa na tujitegemee basi tuwe na bajeti ujamaa,na kama tumeamua kujitegemea tuwe na bajeti ya kujitegemee wote kwa usawa na haki.
Kwa maana gani? Tukiweza kupunguza Bajeti kwenye kundi dogo,na tukaongeza Bajeti kwenye kundi kubwa la watu,katika mzunguko wa hela,kumudu huduma,na ghalaama za maisha,tutakuwa na Bajeti yenye usawa wa maisha.
Jambo la pili,Bajeti imesisitiza kujikita katika uzalishaji,shabaha ni kutoa fursa ya ajira kwa vijana,Sekta ya uzalishaji,Kilimo,uvuvi,Nishati,ufugaji nk,ni eneo muhimu kwa Maendeleo ya nchi na wananchi wenyewe,ni eneo lenye uwanja mpana wa kuajiri nguvu kazi iliyo nje ya soko la ajira.
Maisha ya Mtanzania yapo katika uzalishaji,Maendeleo ya nchi yanategemea uzalishaji wa tija,na hili tuzalishe kwa tija,yaani tuwe na akiba na tuweze kuuza lazima Bajeti ijenge viwanda vya kuchakata bidhaa,Bajeti iajiri nguvu kazi ya kuendesha viwanda hivyo Ili iguse uhalisia wa maisha ya kila Mtanzania.
Kama tunandaa Bajeti,na nguvu kubwa imewekwa katika kujenga miundombinu,ama Kuboresha huduma za jamii,pasi na kiwepo mazingira rafiki ya mwananchi kumudu huduma zenyewe, tutakua tunafanya makosa makubwa ,ikitokea jamii ikashindwa kulipia huduma ya afya,maji na huduma zingine,Bajeti haitakua na uhalisia wa maisha.
Bado tutaamumiza mtozwa kodi ambaye anatumia kiasi kikubwa kulipia kodi kuliko kile anachokipata.
Bajeti yenye uhalisia wakuistawisha nchi na wananchi wake Haina budi kumuwezesha mwananchi mwenye kisomo na asiye na kisomo kuzalisha kwa tija na kulipa kodi.
Tukumbuke,hatuwezi sema tunaendelea tukiwa na uduni wa maisha ya mmoja mmoja,maendeleo upimwa na ustawi wa wananchi wake.
Kama tunajenga hospitali kwa ghalaama kubwa,alafu tuna mwananchi hawezi kumudu huduma hiyo,tunasemaje tumepiga hatua?
Tunafahamu,Mkakati wa Bajeti,ni kutekeleza Mpango wa tatu wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano.
Pili kujenga uchumi shindani na viwanda,pia kuongeza Kasi ya Kufufua Uchumi na Kuimarisha Sekta za Uzalishaji kwa ajili ya Kuboresha Maisha.
Ikiwa hili ndio lengo kuu,sawa,lakini tujiulize,kwa kiasi gani tumewanda wazalishaji, kisera, uwezeshwaji, kuzalisha tija tufikie katika uchumi shindani? Tuna wakulima wangapi wamepewa pembejeo,?tuna wasomi wangapi wakilimo na hawalimi? Tuna wataalamu wa kuchimba nishati ya gesi?tuna wavuvi wangapi wanafanya uvuvi wa kibiashara? Ni lazima tujihoji.
Kama tuna kundi dogo ndio linaendesha uvuvi wa kibiashara na kuachia kundi kubwa wakivua kiholela na kuuza kiholela,bado tumeikosea bajetii na wavuvi,badala yake tunazalisha kidogo na tunauza kidogo.
Sekta ya uzalisha ndio chachu ya uchumi shindani kama tu bajeti itazingatia ushirikishwaji wa wakulima katika kuzalisha tija,kutumia nguvu kazi isiyo katika soko la ajira.
Shabaha ya kujenga viwanda,ni jambo jema,ikiwa tu viwanda hivyo vitabeba uhalisia wa kujenga uchumi,ikiwa itazingatia mahitaji ya nchi,tunahitaji viwanda vya kuzalisha nini?tunahitaji nguvu kazi kwa kiwango gani?lakini tunahitaji nishati ya umeme kiasi gani?
Kama ni mkakati wa Bajeti kuwa na uchumi wa viwanda, pia Bajeti iwe na mkakati wa kuboresha elimu ya ufundi, Bajeti ifufue viwanda vya urafiki na Mwatex na iwekeze kwenye mazao ya kimikakati, Ili iweze kuzalisha malighafi kwa tija tuweze kuuza, na kupunguza ongezeko la Nguvu kazi iliyo nje ya ajira rasmi, hatimaye jamii iweze kustawi.

Upvote
0