Afrolink-Tz Consult Ltd
JF-Expert Member
- Feb 25, 2018
- 424
- 950
Habari za leo!
Tumekuwa tukipeana na kushauriana juu ya mawazo mbalimbali ya kuanzisha shughuli za uwekezaji. Ni jambo zuri na jema kabisa kwa afya ya uchumi wetu kwa mtu mmoja mmoja na hata kwa maendeleo ya Taifa letu.
Katika kupeana mawazo na aina za biashara ambazo kila mtu anashauriwa kuanzisha kipaumbele kikubwa ni biashara ambazo zinaleta faida kubwa na hili ni jambo jema ila wengi wa wanaoleta mawazo haya ya biashara wamekuwa hawaweki wazi kuwa hizi ni biashara nzuri lkn zina “high risks” katika kupata faida iwapo kuna jambo lolote litatokea ambalo linaweza kuwa nje au ndani yauwezo wako kulizuia
Uwekezaji tunaoangalia hapa ni halali tu na si haramu. Hivyo biashara haramu hazihusiki kabisa hapa
Kwanza tuone “risk” (hatari) ni nini? ni ile hali ambayo kuna uwezekano wa kutokea hatari, tishio, tukio au jambo ambao kuna uwezekano wa kushindwa kulizuia hivyo kuleta madhara ambayo yanaweza kuleta hasara/uharibifu
Ieleweke pia, uwekezaji wowote una “risks” zake lakini zinatofautiana kwa kiwango. Vilevile inawezekana ukawa wafanya biashara hizi kwa mafanikio makubbwa lkn ukiangalia vema kuna mambo unafanya kuthibiti “risks” hizo. Hivyo kutokukutokea kwa tatizo haina maana kwamba hilo jambo halipo.
Biashara hizo ni kama ifuatavyo:
1. Biashara za vyakula vibichi
Biashara hizi zina faida sana kama utapata eneo ambalo kuna mzunguko mzuri. Biashara hizi zinajumuisha vyakula vya kupika, mali mbichi kama matunda nk katika masoko nk.
“Risks’ zake:
Biashara za aina hii kwanza zinataka ustadi mkubwa sana hata wakati wa kuzianzisha japo ni rahisi sana. Faida zake huwa ni ndogo ndogo lakini tukitegemea kuuza kwa wingi wa bidhaa tofauti tofauti kwa mtumiaji wa mwisho.
“Risks zake”
Ni biashara zinazoonekana ni rahisi sana kuanza iwe kama ‘website, platform et al. Lakini zinachangamoto kubwa sana kuzisimamisha
“Risks zake”
4. Biashara za jumla
Biashara za aina hii ni rahisi sana kuanzisha pia na kama upo katika eneo sahihi unaweza kufikia kiwango cha juu sana cha mafanikio. Lakini una changamoto nyingi sana
“Risks zake”
Unathibiti vipi ‘risks’?
Waweza kuongeza biashara unayofanya ukatuwekea Risks zake na namna gani unapambana na hizo risks katika kuulinda mtaji wako. Tusiishie tu kutaja au kutoa mawazo ya biashara na kuwashawishi wawekezaji wenzetu kuwa biashara fulani ni rahisi sana wakati umemficha magumu unayopambana nayo kufikia mafanikio.
Karibuni…..

- Muda wa kudumu katika hali nzuri na inayofaa kimatumizi ni mfupi hivyo unapokosea ‘timing’ katika kuvuna na mauzo una hatari kubwa ya kuupoteza mtaji wako. Mfano wakulima wa mazao ya kilimo bidhaa mbichi
- Magonjwa ya milipuko kuzuia biashara isiendelee kwa muda hivyo kuathiri kipato chako na kuharibu mtirirko wa wateja kuja kupata huduma. Mfano ktk migahawa na mahoteli
- Masoko yasiyo ya uhakika hasa kwa Tanzania
- Jitahidi kutafuta soko mapema la uhakika ukijua wazi unatoa mzigo shambani na kuupeleka soko la uhakika tayari mauzo
- Hoteli na migahawa mingi kwa sasa kuna utaratibu wa ukifika unaagiza ndiyo muda huo huo unaandaliwa chakula utakacho kutokana na oda yako. Japo jambo hili linawakera wateja lkn linasaidia kupunguza hasara
- Tujitahidi kuwa na mtandao mpana wa kimasoko, kuwa na takwimu za wateja tunaowahudumia kwa siku (mahoteli, migahawa), kuwa na wateja wa uhakika kwa kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara nk
Biashara za aina hii kwanza zinataka ustadi mkubwa sana hata wakati wa kuzianzisha japo ni rahisi sana. Faida zake huwa ni ndogo ndogo lakini tukitegemea kuuza kwa wingi wa bidhaa tofauti tofauti kwa mtumiaji wa mwisho.
“Risks zake”
- Ushindani mkubwa sana kwani ni rahisi sana kuanzisha biashara za aina hii
- Faida ya bidhaa ni ndogo hivyo bila kuwa makini huwezi kusimama
- Zinahitaji uzoefu mkubwa kiuendeshaji hasa ktk kuchagua soko na bidhaa
- Zinahitaji mtaji mkubwa kufanya biashara iwe na mvuto kutokana na uwepo wa bidhaa tofauti tofauti. Mfano duka la rejareja
- Rahisi kupoteza mtaji kwa kupata bidhaa zisizokidhi viwango kwa wateja. Mfano Biashara ya rejareja ya mitumba
- Andaa muundo, mfumo na aina tofauti tofauti za uuzaji, malipo na ufikishaji bidhaa kwa wateja
- Hakikisha unapoanzisha biashara za rejareja liwe eneo sahihi kwa biashara hii
- Hakikisha unaendana na misimu ya mauzo kwa bidhaa husika
Ni biashara zinazoonekana ni rahisi sana kuanza iwe kama ‘website, platform et al. Lakini zinachangamoto kubwa sana kuzisimamisha
“Risks zake”
- Usalama wa pesa kwa mteja umekuwa wa mashaka sana hasa kwa nchi zinazoendelea. Hii inafanya kuongeza wasiwasi wa matumizi katika manunuzi
- Elimu kwa watumiaji inahitajika hivyo kuwa kwa watu maalum tu ilhali gharama za uendeshaji zipo juu hivyo kupoteza mtaji wake
- Kutotembelewa na wateja wapya hivyoinahitaji kuwa na juhudi za maksudi kutangaza la sivyo unaweza poteza mtaji wako
- Uhakika wa kupata utakacho kwa wakati nayo nihatari nyingine inayomnyemelea mteja
- Usalama wa bidhaa zinazouzwa katika mtandao kuwa si za kuaminika zaidi hivyo kuharibu sifa ya mtandao mzima. Mifano kwa Tanzania ipo mingi sana
- Thibiti wauzaji wa bidhaa kama una “access” nao hasa usalama wa bidhaa
4. Biashara za jumla
Biashara za aina hii ni rahisi sana kuanzisha pia na kama upo katika eneo sahihi unaweza kufikia kiwango cha juu sana cha mafanikio. Lakini una changamoto nyingi sana
“Risks zake”
- Ni biashara zenye faida ndogo sana hivyo kunahitaji umakini wa hali ya juu sana kuhakikisha inasimama
- Ni biashara inayohitaji mzunguko mkubwa na wa uhakika katika mauzo, tofauti na hapo kustawi kwake ni kugumu sana itakukata mtaji
- Eneo la kuanzisha biashara hii ni miongoni mwa mambo ya kuzingatia sana kusukuma mzunguko
Unathibiti vipi ‘risks’?
- Fanya uchunguzi wa kutosha kabla ya kuanzisha biashara aina hizi