Makala nzuri kuhusu ushiriki wa Libya CECAFA, hii ni aibu

ZE NDINDINDI

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Posts
1,885
Reaction score
4,012
kama kawaida wapingaji,watetea waarabu watakuja na kusema labda Salehe jembe alinyimwa kazi Azam au anamuonea wivu bakhressa au watamuambia hao blacks walifata nini libya?

Tusisahau Morocco walivyokataaga na kujitoa dakika za mwisho kuandaaa Afcon eti wanaogopa kupelekewa Ebola na watu weusi....




KUMEKUWA na maandalizi makubwa kuhusiana na michuano ya Cecafa ambayo imepangwa kufanyika nchini Kenya.

Michuano hiyo inaanza Jumapili katika makundi mawili na inaonekana Zanzibar na Tanzania Bara wamejiandaa vilivyo kuhakikisha wanafanya vizuri.
Ukitulia utasikia kuhusiana na michuano hiyo, kila upande ukizungumzia maandalizi na kujigamba kufanya vizuri ndani ya michuano hiyo.

Michuano hiyo kwangu huiona kama haina maana sana na iko kwa ajili ya watu wachache na si mpira wa Afrika Mashariki na Kati.
Kati ya watu ambao nawaona ni chanzo kikubwa cha kudorora michuano hiyo ni Nicholas Musonye ambaye ameamua kuwa kiongozi wa maisha wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Musonye amejiwekea ukuta, ameamua kubaki kama mmiliki wa Cecafa na kuendelea kufanya anavyotaka yeye na si kuangalia maendeleo ya mchezo huo katika ukanda.
Napinga sana hasa kwa viongozi wa mashirikisho ya soka katika ukanda huu ambao nao wanaona mambo yamekuwa ni kawaida tu na wanaonekana pia huenda wanaunga mkono hilo.

Kama wangekuwa hawaliungi mkono, basi wangelifanyia kazi. Cecafa inahitaji mawazo mapya ili kufanya mambo kulingana na wakati tulionao. Ninaamini wanaweza kulitafakari tena jambo hilo kwa kulifanyia kazi.




Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inapeleka timu mbili katika michuano hiyo. Tanzania Bara na ndugu zao Zanzibar ambao ni wapinzani wakubwa wanapokutana.
Tanzania Bara itarusha karata yake kwa kuivaa Libya kama timu mwalikwa katika michuano hiyo. Hakika niwe wazi bila ya kupindisha mambo kwamba napinga kabisa kuiona Libya ikiwa katika michuano hiyo.

Huu ulikuwa wakati wa kuonyesha msimamo wa Kiafrika na kuwaonyesha Walibya kwamba wameshindwa kuonyesha uanadamu kwa kitendo walichowafanyia wahamiaji mbalimbali.

Wahamiaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika wamekuwa wakiuzwa kama watumwa nchini humo. Tayari baadhi ya nchi mbalimbali na hasa za Ulaya zimekuwa zikilaani kuhusiana na tukio hilo. Kwetu Tanzania inawezekana halijatugusa sana, lakini si suala la kuliacha lipite kirahisi hivi.

Libya watakaocheza dhidi ya Kilimanjaro Stars hiyo ya Jumapili wanatokea nchini Libya ambako Waafrika kutoka Afrika Magharibi walikuwa wakiuzwa kama nyanya na Waafrika wenzao kutoka Afrika Kaskazini.

Kuna ‘mentality’ imejengeka kwa watu wengi wanaoishi Afrika Kaskazini kwamba wao wako Ulaya. Wakati fulani tukiwa Cape Verde na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, tuliimbiwa nyimbo zikieleza kwamba wanatuogopa tutawaambukiza ugonjwa wa Malaria.
Nimeona nikiwa Misri, pia Tunisia. Huenda hata hao watu wa Libya walifanya unyama na upuuzi huo wakiamini wao si Waafrika na huenda wanatokea Ulaya.

Kitu kizuri cha kuthibitisha wao ni Waafrika, wanacheza michuano chini ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) na sasa wamealikwa Afrika Mashariki na Kati na wala si upande wa Bara la Asia au Ulaya. Kwao, linaweza kuwa funzo namba moja kama kigezo cha kuiheshimu Afrika na Waafrika.

Hii inaweza isitoshe, nasisitiza, ungekuwa uwezo wangu wangeondolewa mashindanoni ili wafikishe ujumbe kwa wale wapuuzi wa nyumbani kwao walioamua kuwauza ndugu zetu kama vitunguu au maembe sokoni.

Najua Cecafa ni wafanyabiashara, hawawezi kuingia katika jambo hilo hadi lingekuwa na faida kwao kama sasa kupeleka mashindano Nairobi ili kuonyesha Kenya kuna amani ya kutosha na wao itakuwa faida kubwa kwao ukizingatia Musonye ni Mkenya.

Ajabu ni kushindwa kuona ubaya wa Libya, kushindwa angalau kukemea na ikiwezekana kuchukua hatua. Kwa kuwa Libya wanashiriki, basi iko sababu ya ujumbe wa Waafrika kufikishwa kupitia kwao ikiwezekana kwa kuwaonyesha upendo kuliko wanavyotarajia au kuwatuma kwa maneno kwenda kuwaeleza wale wajinga wa nyumbani kwao kwamba, ni lazima kuuheshimu utu wa mwanadamu na Afrika zaidi ni upendo na si upuuzi wanaofanya.

NA SALEH ALLY
 
Kwa nini wasilaumiwe hawa wahamiaji haramu,kuingia nchi za watu bila kufuata sheria?Hasa kwa nchi,ambayo haina utawala wa ukamilifu,ikiwa na waasi wengi.Wahamiaji kama hawa,walioingia Libya,wakati wa utawala kamili,wa Ghadaf walirudi mwakwao matajiri,wamejenga majumba ya ghorofa na makampuni ya biashara.Libya kwa sasa haiwezi kulaumika,nchi iliyoingia vitani,na bado hakujatulia,vipi mgeni unaweza ku jipeleka.
 
acheni mpira uchezwe mbona hasemi nchi zingine ziigomee zanzibar kwa ubakwaji wa demokrasi tuliopata ushuhudia, mbona hamsemi watu wagomee kucheza na tanzania bara kwa ukatili wa kutaka kumuua lissu hadi leo anaangaika hospitali huko kenya? mbona hamsemi tz igomewe kwa mmonyoko wa maadili wanawake wanataka oana wenyewe? vipi kuhusu miili ya wasio na hatia kuokotwa baharini? tuache unafiki, mpira acha uchezwe tukianza kutafuta uovu, hakuna nchi hisiyo na maovu.
 
Duuh ni aibu kuona mtu anatetea libya kwa kigezo chochote kila haifai kuuza binadamu wenzako kama maembe sokoni
 
Duuh ni aibu kuona mtu anatetea libya kwa kigezo chochote kila haifai kuuza binadamu wenzako kama maembe sokoni
Wakulaumiwa ni hao ahamiaji haramu,waliongia kwenye nchi yenye vita,hakuna utawala uliyokamilika,waasi ndio wansofanya mabaya mengi,pamoja na hayo ,sio serekali.
 
kwaupande mwingine wahamiaji haramu wanaokimbilia libya nchi yenye machafuko, wanaenda kutafuta nini huko.
 
Kwanza niwahakikishie saleh ally hana upeo wa kuyaandika hayo pili serikali ya libya haiusiki na kinachoendelea kwenye hiyo biashara tatu waambieni hao magolo watulie nchini kwao
 
Cecafa ya Musonye ni taka taka kabisa, hawajitambui
Watanzania ni wanafiki wakubwa nyie!Yaani kupinga biashara ya utumwa Libya mnamuachia Musonye lawama??!!!Yaani nchi inajua inakwenda kucheza na Libya imenyamaza,viongozi wetu wa kisiasa wamenyamaza,viongozi wa dini kimya,halafu mnataka Musonye ndiyo awe wa kuwapigania waafrika??!!!!Na ndio maana sishangai watu kama ninyi ndio mliojaa humu nchini kulaumu upinzani haujaleta maendeleo!!!!Mbona mnaonesha akili ipo kiwango cha chini saana?
 
Acha wapige ball vijana tupo tunaofatilia hii michuano...asiependa akae pending asubiri world cup mwezi June.
 
Reactions: ywf
kwaupande mwingine wahamiaji haramu wanaokimbilia libya nchi yenye machafuko, wanaenda kutafuta nini huko.

Mleta uzi halioni hilo!!! Alaf anamsingizia Saleh jembe ndie kaandika...mleta uzi analake jambo sio bure.
 
Reactions: ywf
Wakulaumiwa ni hao ahamiaji haramu,waliongia kwenye nchi yenye vita,hakuna utawala uliyokamilika,waasi ndio wansofanya mabaya mengi,pamoja na hayo ,sio serekali.
Wewe dini huwa inakufanya usione ukweli, biashara inafanyika libya unasema haina utawala, je wameweza vipi kuandaa timu ya taifa, kuweka kambi na kushiriki cecafa??
 
Wewe dini huwa inakufanya usione ukweli, biashara inafanyika libya unasema haina utawala, je wameweza vipi kuandaa timu ya taifa, kuweka kambi na kushiriki cecafa??

Au kwakuwa wale ni waarabu ndio maana tunawasakama....wazungu wamedumaza akili zetu.
 
Wewe dini huwa inakufanya usione ukweli, biashara inafanyika libya unasema haina utawala, je wameweza vipi kuandaa timu ya taifa, kuweka kambi na kushiriki cecafa??
Hata somalia wana timu ya Taifa,lakini nenda utuletee mrejesho.Vile vile Sudan ya kusini,pia hakujatulia,vipi mtu mwenye akili sawasawa,atakwenda kwenye vita.
Hawa wahamiaji walikuwa wakiingia kabla ya kuangushwa Ghadaf,na wakirudi mwakwao matajiri,kwa vile kulikuwa na serekali ya uhakika,lakini sasa hakuna serekali iliyodhibiti nchi nzima,tumia akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…