Makala: Taratibu za kufunga kampuni ya biashara Tanzania

Makala: Taratibu za kufunga kampuni ya biashara Tanzania

Afrolink-Tz Consult Ltd

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2018
Posts
424
Reaction score
950
Habari za leo!

Napenda leo tuangazie makala hii juu ya taratibu za kufunga kampuni ya biashara hata kama imekuwa katika shughuli za kibiashara kwa miaka mingi

Wafanyabiasha wengi hupenda kufanya biashara kwa mafanikio makubwa katika muundo wa mtu binafsi au washirika au kampuni yenye ukomo. Sasa kuna wakati mambo huwa hayaendi kama ilivyotarajiwa hasa katika njia mbili ikiwa ni ushirika (partnership) au kampuni yenye ukomo (limited company). Sababu zaweza kuwa:
1. Hali ngumu ya kibiashara
2. Usimamizi mbovu hivyo kupelekea biashara kupata hasara
3. Kutokuwepo na maelewano baina ya washirika au wanahisa
4. Kufilisika nk

Sasa baada ya matukio kama hayo ni vema kufunga kampuni au ushirika badala ya kuisusa ambapo madhara yake huwa ni pamoja na:
1. Malimbikizo ya faini zitokanazo na kutowasilisha ritani stahiki kwa wakati stahiki kwa Mamlaka stahiki
2. Ongezeko la kodi mbalimbali nk

Hivyo basi fuata hatua hizi kufunga biashara yako iwe binafsi, ushirika au kampuni yenye ukomo

1. Hakiki nafasi yako kikodi (Tax Position) kutoka Mamlaka ya Mapato - TRA
Hapa ni lazima uhakikishe kuwa huna deni lolote. Faida ya "Tax position” utaweza kujua madeni kama yapo ya kodi mbalimbali na hivyo kufanya maamuzi sahihi ya kulipa kwa maramoja au kwa awamu baada ya kuandika barua na kupata mkataba

2. Andaa hesabu za mizania za muda uliohusika kibiashara

3. Wasilisha barua pamoja na barua ya bodi ya wakurugenzi/washirika juu ya maamuzi ya kufunga biashara pamoja na hesabu za mizania katika Mamlaka ya Kodi

4. Omba cheti cha mlipakodi ie Tax clearance certificate kuelekea BRELA baada ya kupata mara baada ya kupata majibu toka Mamlaka ya kodi kama hakuna lolote. Iwapo una madeni bhasi waweza fanya taratibu za kuomba kulipa kwa awamu then ukimaliza unaomba cheti

5. Ukimaliza Mamlaka ya Kodi - TRA basi unahamia Wakala wa usajili biashara na leseni - BRELA. Hakikisha huna ritani unayodaiwa katika mfumo wa ORS

6. Andika Barua ya azimio la kuifunga kampuni/ushirika na kuutangaza ktk gazeti la serikali na magazeti mengine ya maana (sio ya udaku). Nakala za magazeti haya hakikisha unazipata na kuzitunza vema kwani zitahitajika ktk hatua inayofuata

7. Wasilisha barua ya kufunga kampuni, barua ya bodi ya wakurugenzi/washirika (Special resolution), nakala ya gazeti la serikali na magazeti mengineyo ya tangazo la kuifunga kampuni pamoja na fomu za kufunga kampuni kutoka BRELA

8. Kama kila kitu kipo shwari baada ya siku 90 utapata majibu ya uthibitisho wa kufungwa kwa kampuni/washirika

Nimejitahidi kuandika kwa kifupi kuepuka kuwachosha.

Pia wajuzi karibuni kuongezea zaidi wote tupate kuwa na elimu hii

Kwa maswali, maoni na ushauri karibuni sana
 
Back
Top Bottom