Makala ya mwisho ya Padri Privatus Karugendo kwenda gazeti la Mwananchi siku 2 kabla ya kufariki

Makala ya mwisho ya Padri Privatus Karugendo kwenda gazeti la Mwananchi siku 2 kabla ya kufariki

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
1,730
Reaction score
2,230
Wakati Rais Samia Suluhu Hassan, anatimiza siku 100 akiwa madarakani, ni wazi Watanzania bado wana kiu ya kupata Katiba Mpya.

Na wengi hususan wanasiasa, wamekuwa wakiidai kwa nguvu zote.

Hata hivyo, itakumbukwa wakati Samia anaapishwa kuwa Rais, alisema anajua kuwa miongoni mwa mahitaji ya Watanzania ni Katiba mpya, “lakini wasubiri kwanza.”

Pamoja na kauli njema hiyo ya mama, ni vyema tukatafakari kidogo. Maana kuna watu wana mawazo kwamba tunaweza kutengeneza Katiba vijiweni!

Pia kuna mawazo potofu yanayoendelea kwamba kila mtu ni mtaalamu wa kutengeneza Katiba.

Wengine wanafikiri Katiba ni kama Mahakama na wengine wanafikiri Katiba ndiyo jibu la kila kitu.

Jibu la Rais Samia kuwa tusubiri kwanza, lina maana kubwa na Watanzania wanapaswa kulitafakari kwa kina.

Vinginevyo tutachanganyikiwa hata kabla ya kumaliza kazi yenyewe ya kutengeneza Katiba hiyo.

Na swali la kujiuliza jingine ni je, tunaitaka Katiba ya vivuli au Katiba ya vitu halisi?

Tujiulize, tunaitaka Katiba ya kuwalinda watu fulani, au kukipendelea chama fulani cha siasa au kuipendelea dini fulani?

Ni wazi majibu yatakuwa hapana, bali tunataka Katiba ya wananchi.

Inawezekana leo ninaelekea kujadili mada inayochanganya kidogo, wakati Mama yetu ndiyo kwanza ana miezi mitatu tu na siku 10 madarakani.

Lakini ili kuijadili vizuri mada hii, nitamtumia mwanafalsafa Plato, aliyeona kwa mara ya kwanza ukweli juu ya vivuli na vitu halisi.

Plato ndiye mwanafalsafa aliyeanzisha Astria ya Pango. Asria hii ndiyo iliyoendelea hadi kuonyesha ukweli kwamba kuna vitu vinavyodumu na vile vinavyopita. Kwamba vingine ni vivuli na vingine ni vitu halisi, ukweli na vitu visivyobadilika milele yote. Mfano, upendo ni kitu kinachodumu milele yote.

Watu wanaopendana wanakuja na kupita, lakini upendo upo palepale. Au ubaya. Watu wanatenda ubaya na kushiriki ubaya wanakuja na kupita, lakini ubaya unabaki palepale. Hata kama tungefanikiwa kuwamaliza wabaya wote, ubaya utabaki katika wazo la ubaya, na endapo atachipuka tena mtu mbaya, atashiriki ubaya katika wazo la ubaya!

Hii astaria ya pango ilimfikisha Plato, katika hatua ya nadharia ya mawazo. Hii inajulikana kama nadharia ya Plato ya Mawazo.

Kwa ujumla, nadharia ya mawazo ni ule ukweli ambao haubadiliki au una hali ya umilele na haina hali ya umaada ambapo vitu vyote vijavyo kwetu katika hali ya umaada huja kama vivuli vyake.

Kulingana na Plato, ni elimu pekee yake ambayo inaweza kuwatoa hawa watu kutoka kwenye maisha ya kivuli kwenda kwenye ulimwengu wa mwanga.

Elimu kadiri ya Plato si tu jambo la kusoma vitabu mbalimbali na kupata shahada, bali ni hali ile inayomfanya mtu awe na uwezo wa kujua ukweli kama ulivyo na kuishi kadiri ya misingi ya hiyo elimu. Kwa kadiri ya Plato, elimu ni lazima imfanye mtu abadilike kutoka kwenye ulimwengu wa kivuli na kwenda kwenye ulimwengu wa mwanga. Na kwamba mtu akishapata mwanga, atakuwa hajapata elimu ya kweli kama hatachukua jukumu la kuwafundisha wengine.

Kwa maneno mengine, mtu mwenye elimu ya kweli ni yule anayeipata elimu akatoa elimu. Mtu anayeipata elimu akabaki nayo anakuwa bado yuko gizani, pangoni!

Mtu, aliyeelimika ni yule anayeshughulika na vitu visivyopita. Ni mtu yule anayeshughulikia heshima, kuliko kushughulikia watu wanaoheshimiana, ni mtu anayeshughulikia upendo kuliko wapendanao, na ni yule anayeshughulikia Utanzania kuliko kuwashughulikia Watanzania!

Si kwamba anawapuuza Watanzania, hapana, ila kwake kitu cha msingi ni Utanzania. Mtu anayetanguliza Utanzania, atawahudumia Watanzania wote bila kuangalia kabila, sura, cheo au hali ya mtu.

Mtu, anayetanguliza Utanzania, atatenda haki wakati wote, atawapenda Watanzania wote na atawahudumia wote. Sote tukishughulika na Utanzania, Tanzania yenye neema inawezekana leo, kesho na keshokutwa. Tanzania yenye neema kwa vizazi vijavyo inawezekana pia! Hivyo ni muhimu kwetu sote kukazana kuisaka elimu, elimu ya kweli ya kutuletea mwanga na kututoa gizani.

Hoja pana ni kwamba, kama tunatengeneza Katiba ya vivuli itadumu muda mfupi na kutokomea kusikojulikana. Lakini kama tunatengeneza Katiba ya vitu halisi; mfano Katiba ya upendo badala ya wapendanao; Katiba ya heshima badala ya wanaoheshimiana; itadumu vizazi na vizazi.

Nina imani Rais Samia anapoendelea na majukumu yake, ataendelea kufikiria namna njema ya kuufufua na kuuendeleza mchakato wa kutafuta Katiba Mpya uliokwama, ili kukata kiu ya Watanzania.

Ni vyema kuwashirikisha watu wote juu ya Katiba. Ni vyema kwamba makundi mbalimbali yakatoa maoni juu ya Katiba. Lakini ni lazima tufike mahali tukubali kwamba si kila mtu anaweza kutengeneza Katiba.

Privatus Karugendo

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Huyu upo uwezekano akawa ni huyu mwana JF aliyefariki majuzi hapa akitumia jina la kike humu?

Lipo bandiko lake humu akiaga kwa uchungu content yake mwanzo mpaka mwisho alikuwa anazungumza sana issue ya katiba,Mungu amrehemu.
Ni huyohuyo hayati Privatus Karugendo. Alijiita Beatrice Kamugisha. Alikuwa mtu wangu wa karibu wakati nipo Dar kabla ya kuondoka rasmi 2011, lakini tulikuwa tunawasiliana.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Kwani amefariki kweli? Yule Beatrice Kamugisha ?

Kuna uzi juzi jioni ulikuwa una-trend sana humu ndani ya 24hrs ukizungumzia kifo cha member mwenye jina ulilotaja hapo juu na ukiusoma huo uzi kwenye link hapo juu aliou-post siku tatu nyuma maudhui yake na alichoandika hapa havijapishana sana nadhani mods baada ya kuona wadau wameunga unga dots hadi kuhisi ni yeye wameuondoa ule uzi wa kifo ili kulinda privacy yake.
 
Mbali na masuala ya siasa, alipigania sana haki ya mapadri kuoa kinyume na imani yake ya kikatoliki. Aliamini sana kuwa ndoa ni jambo jema kwa mapadri. Alidhani angeleta mabadiliko kwenye madhehebu hayo lakini akagonga mwamba, akatengwa na kuamua mwenyewe kuoa huku akiwa muumini wa kawaida.

Alikuwa rafiki yangu sana na mkewe Rose aliwahi kukaa kwangu kabla hawajaoana rasmi. Mahusiano yao yalikolea tangu akiwa padri chini ya Askofu Severine NiweMugizi. Walikuwa na upinzani mkali na Askofu wake huyu na sijui kama waliwahi kupatana. Kabla ya kupishana na NiweMugizi alikuwa chini ya Askofu Mwoleka

No, nazungumzia Beatrice Kamugisha not Padre
 
Mahusiano yao yalikolea tangu akiwa padri chini ya Askofu Severine NiweMugizi. Walikuwa na upinzani mkali na Askofu wake huyu na sijui kama waliwahi kupatana. Kabla ya kupishana na NiweMugizi alikuwa chini ya Askofu Mwoleka

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app

Mara kadhaa nimekisoma kisa cha huyu Muheshimiwa,nadhani au niseme huyu hakuwa na upinzani na Ask Niwemugizi binafsi bali na taasisi nzima Catholic,angekuwa popote lililompata kutoka kwa Niwemugizi lingemkuta tu kwa sababu ni sheria za taasisi siyo za mtu mmoja

Hata kama alijiona ana haki ya kuishi anachokiamini alitakiwa aende kwa taratibu zinazotakiwa haiwezekani unaambiwa jambo fulani mipaka yake ni hapa kisha wewe kwa sababu unajiona unatosha ukaamua kufanya alimradi bora liende....kama ulivyosema akiwa bado Padre alikuwa na mahusiano na mwanamke mpaka wewe ukajua obviously alijua anakosea kutokana na siyo utaratibu wa kiapo alichokiapia.

Siyo muda wa kumlaumu tumuache apumzike.
 
Umesema ukweli. Alikuwa na misimamo mikali sana ilibidi nikubali kutofautiana naye kwa mambo mengi. Baadaye hata kuoa wake wengi (polygamy) aliafiki!!!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom